Ubumuntu
JF-Expert Member
- Oct 21, 2010
- 14,345
- 10,885
Salaam,
Wakati mamsapu alipokuwa mjamzito, nilikuwa nikienda nae kliniki mara kwa mara. Sasa siku moja, katika mazungumzo, nikamsikia dada mmoja aliyekuwa ana mtoto mchanga hapo kliniki, akisema daktari wake alimwambia sababu ya mtoto kufanana sura na wazazi wake.
Alisema kwamba, daktari alimwambia kwamba: mtoto anapofanana sura na baba, ina maana wakati wa tendo la ndoa (na muendelezo wa mbegu ya kiume kukutana na ya kike), mama aliridhika, kwamba, mama alifurahia tendo na kuridhika kabisa. Na pale mtoto anapofanana na mama ina maana mama hakuridhika kabisa, kwamba, baba alimwacha mama njiani.
Nilibaki na butwaa!! Dah! Ikabidi niwe nasubiria kwa hamu kufahamu mtoto wetu atafanana na nani. Ile kuzaliwa tu, kulalaleki, kidume kikawa kinafanana na mimi kama copy and paste!
Sasa, ninaandika haya, ili kuweza kupata ujuzi wa JF Doctors.
Hili suala la ukweli wa kisayansi ama yule daktari alimchengua tu yule dada?
Maana najiuliza, iwapo mtoto anafanana na wazazi wote, hapo inakuaje?
Wasalaam.