Je, Hii ni hali ya kawaida?

Vitalis Msungwite

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2014
Posts
3,292
Reaction score
7,867
Mwezi wa tano ilifunguliwa kesi ya rufaa katika mhakama ya wilaya ya Mbarali kutoka mahakama ya mwanzo ya Rujewa umbali wa mita 30. Kesi hii ni ya milathi maana kuna MTU aliidanganya mahakama na mahakama ikampitisha kuwa msimamizi wa milathi. Baada ya kufunguliwa tarehe ya kurudi ikawa June 4.

June 4, mjibu rufaa aliiomba mahakama imuongezee muda wa kujibu rufaa kutokana na kuchelewa kupata samansi. Mahakama ikapanga June 24 ndio siku ya kurudi.

June 24, baada ya kuripoti wote hakimu akasema faili halijafika toka mahakama ya mwanzo ambayo ipo umbali wa mita 30 tu na zipo kwenye fensi moja. Ikapangwa July 11 iwe ndio siku ya kusikiliza shauri.

Tarehe zikawa hivi July 11, July 25, August 2, August 21, na sasa imepangwa tena September 4. Katika kipindi chote hicho cha kuripoti mahakamani imekuwa ikitolewa sababu moja tu kuwa faili halijafika!!!

Wataalam wa masuala haya tusaidieni mawazo, hii ni kawaida? Maana isije ikawa Mimi ndio ninaharaka. Kama sio kawaida nitatakiwa kuripoti wapi ili mambo yaende?
 
Andika barua kwa naibu msajili wa mahakama kisha nakala kwa mfawidhi wa mahakama hiyo kesi ilipo kisha thank me later
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…