Je, hiki kipodozi ni salama?

kirusi cha ukimwi

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2015
Posts
799
Reaction score
646
Habari yenu wana jamii forum nina dada yangu amenunua kipodozi hiki na hajui kama ni salama au lah na je kinaweza kikuwa na viambata hatati ? ntakuwa mwenye shukran kwa kijuzwa
 
Hii ni sumu hatari sana hasa kwa mama wajawazito
 
Ni vizuri ungepiga picha upande unaoonyesha “Ingredients” lakini kwa sehemu kubwa Skin Lightening zinakuwa na mchanganyiko ambao si mzuri kwa afya ya mtumiaji kama vile Mercury,Hydroquinone ,Lead n.k hizi huweza kupelekea magonjwa kama vile kansa ya ngozi na ugumba
 
Haina Tbs au kama nembo ya TBS ipo basi imehakikishwa kwa matumizi lakini kama hakuna basi ujue kuna madhara
 
Hii vitu hatari sana, si mpake mafuta ya nazi tu ni mazuri ukijipulizia na parfum kidogo inakuwa poa
 
Soma kama kuna haidrokwinini na mekyuri si salama
 
Nje ya mada: Kuna siku nilikutana na dada mmoja hivi tunafahamiana, usoni alikuwa ana mapele makubwa makubwa, nikamuuliza kulikoni? akasema eti alikuwa Dar es Salaam, akiwa kwenye duka la vipodozi akaja Wema Sepetu akanunua hicho kipodozi, basi hapo hapo na yeye akaona hicho ndio chenyewe (kwa kuwa tu kamuona Wema Sepatu kanunua). Alivyoanza kutumia ndio matokeo yake akaota hayo mapele manene manene.
 
Wenzetu kabla ya kutumia vipodozi wanamconsult doctor wa ngozi. Sio kila kipodozi anachopaka mwingine mwingine kitamfaa. Ngozi zetu zinatofautiana. Unaweza nunua kipodozi cha mtu mwenye ngozi kavu kumbe uso wako wa mafuta ukipaka ndo yanatukuta hayo ya najionea makubwa.
 
Ni kweli unavyosema Mzigua90. Yaani nilimshangaa yule dada, mwanzoni nilidhani anatania kumbe ni kweli. hahahahahahaha
 
Habari yenu wana jamii forum nina dada yangu amenunua kipodozi hiki na hajui kama ni salama au lah na je kinaweza kikuwa na viambata hatati ?View attachment 734285 ntakuwa mwenye shukran kwa kijuzwa
Hiki ni kibaya. Sio hiko tu, vipo vingi sana na madhara yake pia yanapatikana katika kitabu SURA NZURI NGOZI NYORORO. Kwa yeyote anayependa kuna muongozo kamili, free copy (soft copy), ya orodha ya vipodozi visivyo salama na madhara yake A-Z. Ni BURE KABISA, omba sasa na utatumiwa kwa njia ya e-mail. Tuma meseji kwenda namba 0719326693 ili kupata muongozo kamili kwa njia ya email.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…