Kama ni kijembe basi ni kwa Ruby na sio kwa Clouds!
Sioni ni namna gani Clouds wanaathirika kwa ajili ya Jide lakini kwa upande wake, kilichobaki kwa Jide is just a pride... kwamba hawezi kupiga magoti!! Ni kama zile historia za akina Mkwawa... kuliko kukamatwa na Mjerumani baada ya kuwa ameshashindwa vita, basi ni bora ajiue!!!
Na kama ni kijembe kwa Ruby, what for?! Keshakuwa mtu mzima sasa na keshapita rika la kusutana na vitoto mitandaoni bila sababu za msingi!! Ruby ni mdogo sana kitasnia...
So, busara kwa JD ilikuwa ni kum-mentor Ruby kuliko kumpiga vijembe!! Na moja ya mentorship ni kumwambia wazi kwamba "Ruby, wewe bado ni mdogo sana kuanza kuvimba kichwa... haya mambo tuachie sisi!"