Je!historia inasemaje juu ya mwanadamu yesu?

Je!historia inasemaje juu ya mwanadamu yesu?

st44273

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2013
Posts
341
Reaction score
137
Yeye Ni:
  • Mtu wa ajabu kupita watu wote katika nyakati zote za historia ya mwanadamu
  • Mtu aliyejitokeza kuwa mashuhuri kwa vipindi vyote
  • Mwalimu mkuu,mtu aliyefanya matendo mema kwa wanadamu kupita mwingine katika historia
  • Mtu aliyeishi maisha matakatifu kuliko yeyote aliyewahi kuishi duniani

Tembea sehemu yoyote ulimwenguni. Ongea na watu wa dini yoyote. Haijalishi jinsi walivyoshikilia tabaka za dini zao, kama wanajua chochote kuhusu historia, watakubali kwamba hakujawahi kuwa na mtu kama Yesu wa Nazareti. Yeye ni mtu wa ajabu mno kuliko watu wote wa enzi zote.Hakika Yesu alibadilisha mwenendo wa historia.

Maisha aliyoishi Yesu, miujiza aliyotenda, maneno aliyosema, kufa kwake msalabani, kufufuka kwake, kupaa kwake mbinguni - yote yathibitisha kwamba yeye hakuwa mwanadamu peke yake bali alikuwa zaidi ya mwanadamu. Yesu alisema, "Mimi na Baba tu umoja" (Yohana 10:30), "Aliyeniona mimi amemwona Baba" (Yohana 14:9).

Mwanahistoria mmoja mashuhuri sana (Lewis) aliandika hivi :
"Mtu ambaye alikuwa mwanadamu peke yake na kusema maneno kama aliyoyasema Yesu hawezi kamwe kuwa mwalimu wa utu wema. Huenda ikawa alikuwa mwenda wazimu - sawasawa na mtu anayesema kwamba yeye ni yai lililochemshwa - au roho chafu kutoka kuzimu. Wewe lazima uchague. Kama yeye (Yesu) alikuwa, na hata sasa ni Mwana wa Mungu, au yeye ni mwenda wazimu au kitu kibaya zaidi. Unaweza kumwita mpumbavu au unaweza kujinyenyekeza chini ya miguu yake na kumwita Bwana na Mungu. Lakini tusije na maneno hohehahe tukisema kwamba yeye alikuwa mwalimu shupavu wakibinadamu tu."

Hii inaleta kwenye hitimisho kuwa,hakika Yesu ni zaidi ya mwanadamu,ni zaidi ya nabii,historia inadhibitisha kuwa Uungu wake si kitu cha kutilia shaka.

Ubarikiwe.
 
Back
Top Bottom