Je, homa ya ini inatibika kwa mitishamba?

GRAMAA

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2014
Posts
1,241
Reaction score
3,800
Ipo hivi wakuu, kuna ndugu yangu ana tatizo la HOMA YA INI(Hepatitis B) kwa muda mrefu sasa zaidi ya miaka kumi sasa ila ukimcheki yupo fresh tu.

Tulienda Muhimbili akapimwa akapangiwa clinic kwa muda mrefu sana ila kila akipimwa anaonekana yupo positive.

Sasa kuna daktari mmoja pale Muhimbili akatushauri tujaribu kwenye miti shamba kwani Hospital hakuna dawa ya hili tatizo.

Baada ya kushauriwa hivyo, tukaanza kufanya upelelezi kama ni kweli hili tatizo linatibika kwa Miti shamba au ndio tusubiri tu umauti.

Katika pitapita yetu YOUTUBE tukakutana na wataalam mbalimbali waliojieleza kuwa wao wanatibu HOMA YA INI kwa miti shamba.

Hofu inakuja bongo wapigaji wamekuwa wengi sana inatupa shida kuamini moja kwa moja.

Wakuu najua humu kuna watu wengi sana na wengine watakuwa na ushuhuda wa hili tatizo kama linatibika kwa miti shamba au laa.

Je, HOMA YA INI inatibika kwa miti shamba kweli?
 
Andika sasa hivi mkuu maana hali ni mbaya
Dawa yake ni kama ifuatavyo hapa

1: Unga wa majani ya phylanthus(maarufu kama mzalia nyuma ) vijiko 12 v
2: Unga wa manjano iwe mpya vijiko 8
3: Unga wa mizizi ya aloevera vijiko 8
4: Unga wa matawi ya masongwe vijiko 8
Changanya vyote kwa pamoja vizuri mpaka upate mchanganyiko mzuri
Matumizi ni kijiko kidogo unaweka kwenye maji ya moto sana unakoroga vizuri unaacha ipoe kunywa kutwa mara 3 ndani ya sku 120 kutegemea ukubwa wa tatzo Mungu atakusaidia utapona


Sent from my Infinix PR652B using JamiiForums mobile app
 
Dawa yake ni kama ifuatavyo hapa
1:unga wa majani ya phylanthus(maarufu kama mzalia nyuma ) vijiko 12 v....
Je, kuna masharti yoyote kipindi unatumia hizi dawa mkuu.

Hasa kwenye upande wa vyakula gani vinatakiwa kuliwa na vyakula gani havitakiwi kuliwa mkuu.
 
Je kuna masharti yoyote kipindi unatumia hizi dawa mkuu.

Hasa kwenye upande wa vyakula gani vinatakiwa kuliwa na vyakula gani havitakiwi kuliwa mkuu.
Kuhusu vyakula wakati unatumia dawa sansana ni kuacha kula vyakula na kunywa vinavyozalishwa viwandani kama soda hzo

Sent from my Infinix PR652B using JamiiForums mobile app
 
Changamoto ni kwenye kuupata tu.

Ngoja tumbane kutafuta hizo package mkuu
Ipo mingi sana mkuu hasa kipindi hiki cha mvua inaota sana kanda ya ziwa kama mwanza na Mara inapatikana ,lkn pia utajarbu kwenye maduka ya dawa za asili unaweza upata unga wake pia kuna mzee pale Mwanza mjni nitamuuliza kama huo unga anao ntakujuza utaupata vipi.

Sent from my Infinix PR652B using JamiiForums mobile app
 
Kuna MTU aliniambia hivyo vijani vyake ni dawa ya presha.
 
Utakuwa umenisaidia sana mkuu.

Kwani hakuna mchanganyo wa hiyo dawa ikiwa kamili mkuu?
 
Utakuwa umenisaidia sana mkuu.

Kwani hakuna mchanganyo wa hiyo dawa ikiwa kamili mkuu?
Kuipata ikiwa kamili ni ngumu sana ila kwenye maduka ya dawa za asili hivyo vitu unapata unaendabtu kuandaa home kwako kwa usafi na umakini zaid hvyo ni bora ukaandaa mwenywe tu.

Sent from my Infinix PR652B using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…