Je, huko waliko vyuma vimekaza au vimelegea?

Elitwege

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
5,294
Reaction score
10,970
Habari,

Sekeseke la kuwabana wakwepa kodi kwa kutumia task force na kufunga biashara zao lilizua mjadala kila kona kwamba hilo zoezi linawasababishia hao wakwepa kodi ugumu wa maisha na vyuma kukaza hivyo TRA wakaamuliwa kuachana nalo.

Sasa TRA wanakusanya kodi kwa kuwabembeleza wakwepa kodi na hairuhusiwi kuwafungia maduka yao maana maisha yatakuwa magumu sana kwao.

Je, hao wamachinga walioondolewa na kufungiwa vibanda vyao, vyuma vimelegea au vimekaza huko waliko? Hela zimejaa mfukoni mwao? Maisha yamekuwa mazuri mno kwao na sasa wanakula kuku kwa mrija?

Hela zimejaa mitaani?

Kama maisha yamekuwa magumu kwao huko waliko nani alaumiwe?

Njaa haina baunsa.

Adui muombee njaa.
 
Kwa sasa we unaenda tra, wakikupa dodoso la malipo mfano millioni 6 we unawaambia mi naingiza mill 1 kisha mill 2 nawapa cash. Umemaliza kesi. Jamaa yangu juzi kamalizana nao kiivyo.
 
Kwa sasa we unaenda tra, wakikupa dodoso la malipo mfano millioni 6 we unawaambia mi naingiza mill 1 kisha mill 2 nawapa cash. Umemaliza kesi. Jamaa yangu juzi kamalizana nao kiivyo.
Inasikisha sana
 
Kwa sasa we unaenda tra, wakikupa dodoso la malipo mfano millioni 6 we unawaambia mi naingiza mill 1 kisha mill 2 nawapa cash. Umemaliza kesi. Jamaa yangu juzi kamalizana nao kiivyo.
1m inaingia serikalini, 2m inaingizwa mtaani kwenye mzunguko watu wanarejeshewa furaha waliyoikosa kwa miaka 5.

Very brilliant.
 
Wacha wenye nafasi wazidi kula.
Maana hata wasipokula hakuna tunachopata.
 
1m inaingia serikalini, 2m inaingizwa mtaani kwenye mzunguko watu wanarejeshewa furaha waliyoikosa kwa miaka 5.

Very brilliant.
Na Ulaya unakoenda kuomba msaada huwa wanafanya hivyo?

Huna akili kabisa
 
Kwahiyo we mbuzi unapingana na mawazo ya Mwenyekiti wa chama chako?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…