Je, huruhusiwi kufanya mtihani wa kidato cha sita kama school candidates kama huna jumla ya total points kwa O Level?

Je, huruhusiwi kufanya mtihani wa kidato cha sita kama school candidates kama huna jumla ya total points kwa O Level?

BWANA MISOSI

Member
Joined
Feb 11, 2020
Posts
39
Reaction score
24
Habari wana JF.

Leo nilikuwa kwenye daladala asubuhi nikasikia mama mmoja analalamika kuwa mwanae amesajiliwa kama private candidate kwenye mtihani wa form six. Sababu anasema kuwa mwanaye hajafikisha points 25 kwa matokeo yake ya form four pamoja na kurisiti, kurisiti, yaani ukichukua jumla za points kwa mtihani wakati amemaliza na alivyorisiti inatakiwa ifika point 25 kwa masomo aliyofaulu.

Tofauti na hapo atasajiliwa kama private candidate, na pia nimemsikia huyo mama akisema kuwa kama kwenye kombi haujabalance kwa kupata credit kwa kila somo hutaruhusiwa kufanya mtihani wa form six as school candidate ila utasajiliwa kama private candidate?

Maana yake kwa sasa huruhusiwa kufanya mtihani as school candidate hujabalance kombi na hujafikisha point 25 hata kama umefanikiwa kupata credit tatu, je ni kweli? na kuna shida gani endapo ukisajiliwa as private canditades? Kitu gani unakosa endapo ukisaliwa private candidate ambacho school candidates anapata?
 
Sifa za kufanya mtihani kwa private na govt school ni moja. Mtu anatakiwa kuwa na credit Yaani C au zaidi tatu. Na kwenye comb yake anayofanyia mtihani hatakiwi kuwa F kwa somo lolote.

Sifa za kusoma private na govt ndio zinapishana. Mtu anaweza kufanya mtihani hata Kama four ilimradi ana sifa but hawez kuchaguliwa kusoma govt

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom