Kig
JF-Expert Member
- Aug 13, 2012
- 1,076
- 458
Kwenye kijiji ninaoishi bei ya trei moja la mayai ni kati ya Tsh 6,000/= hadi 8000/= kutegemeana na msimu. Nimepata wazo nianzishe mradi wa kufuga kuku wa mayai (kuku wa kisasa). Mtaji wangu kiduchu/kidogo unatosha kuanza na kuku 600. Huduma ya vyakula vya kuku na dawa zinapatikana karibu na ninakoishi. Kuhusu mahali pa kufugia kuku, nategemea nibadili matumizi ya jengo ambalo ni jiko liwe banda kwa ajili ya kuku. Nawaombeni na kuwasihi sana mlio na uzoefu wa hii biashara tafadhalini mnipe ushauri kama itaweza kunitoa kimasomaso toka kwenye ukata wa kipato. Maisha magumu balaa!!!!!! Natanguliza shukrani kwa michango yenu ya mawazo. Asante.