Tetesi: JE HUU NI MGAO WA UMEME AU NI MATATIZO YA KIUFUNDI?

Tetesi: JE HUU NI MGAO WA UMEME AU NI MATATIZO YA KIUFUNDI?

Monseur

JF-Expert Member
Joined
Dec 5, 2016
Posts
655
Reaction score
525
Nauliza hivi kwa Sababu nimeshuhudia maeneo mengi ya Dar es Salam yakitawaliwa na kiza kuanzia mwanzoni mwa wiki iliyopita. Kwa mfano majuzi maeneo ya Kigogo mwisho hayakuwa na umeme siku nzima. Jana tarehe 27/10 Makumbusho hakukuwa na umeme.

Na Leo tena tarehe 28/10 Kuanzia mchana hadi Usiku huu navyoandika uzi huu maeneo ya Kigogo Kati yote kilio ni hicho hicho.

Kama ni mgao umerudi kimyakimya ni vyema Mkurugenzi wa TANESCO auhabarishe Uma ili turudi tulikotoka , kwenye biashara ya Magenerator. SERIKALI hii ilituahidi kuwa mgao wa umeme ungebaki kuwa historia, Sasa veeeppe!!!
 
Watakua wanaweka mitambo mipya ya umeme wa gas mkuu
 
Leo Niliona Sehemu Kulikuwa Na Katizo La Umeme Na Tanesco Wakikagua Meter Za Luku
 
Sikumbuki mara ya mwisho umeme ulikatika zaidi ya dakika kumi ni lini....
 
Back
Top Bottom