Je, huu ni ubunifu katika biashara?

Brojust

JF-Expert Member
Joined
Sep 17, 2016
Posts
349
Reaction score
1,024
Salaam wakuu!

Bango hili lipo sehemu nimekutana nalo ni njia panda (Samahani nimezoom simu yangu haijatoa clear).

Naomba kuuliza swali, Je mmiliki wa hii sehemu pendwa kwa ukanda wa vingunguti, gongo la mboto na viunga vyake, na sehemu nyingine ambapo mimi sijafika.

1. Amefanya ubunifu ili matangazo yake yafikiwe na watu wengi?

2. Ameprove wrong kwamba ukiwa na hela kila kitu kinawezekana?

3. Amedharau taasisi hiyo inayomiliki hizo nguzo na kumtuma kijana kwenda kuweka bingo hilo mahali pale huku akijua ni kinyume na sheria?

NB; Asitokee mtu akasema labda namuonea vivu sababu na mimi namiliki sehemu kama hiyo, Hapana, sijawahi kumiliki ila nimeangalia na nimewaza sana aliwaza nini kuweka hilo bango hapo.

Labda wenzangu mna mawazo mengine.

Karibuni sana.
 
Kisheria hairuhusiwi kuweka matangazo kwenye nguzo za umeme, labda kama Tanesco waliruhusu afanye hivo, maana kupanda kwenye nguzo kama hizo kuweka bango kama Hilo inatakiwa umeme uwe umekatwa , huo sio ubunifu ni uchafu
 
Mbona yako mengi hayo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…