Je, huu ni Uthibitisho kwamba Watanzania wanajua mno Kusali au labda wanajua sana Kuroga?

Je, huu ni Uthibitisho kwamba Watanzania wanajua mno Kusali au labda wanajua sana Kuroga?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Corona ilikuwa Tishio duniani na hasa Tanzania lakini ilipotangazwa tu kuwa inakaribia kuja Kutuambukiza na Kutuua kwa Mshangao mkubwa ikatoweka.

Tokea Juzi TMA wanatutisha tu Watanzania ( hasa hasa Wakazi wa Mkoa wa Dar es Salaam ) kuwa Leo tarehe 25 April, 2021 tungekiona cha Mtema Kuni kwa Kimbunga Jobo cha Kushangaza sijui hata Kimepotelea wapi.

Niliwahi Siku moja kumsikia Mzee Mkongwe Mmoja akisema kuwa hakuna Taifa lenye Imani Kali Kimaombi duniani kama Tanzania ila pia hakuna Taifa ambalo Watu wake wanajua Kuroga kwa Kuiomba Mizimu yao kama Tanzania.

Je, Jobo Kapeperushwa Kimaombi ( Kwa Mungu Baba ) au ni Mambo yetu ya Kiutamaduni ( Ndumba Nangai ) tuliyoyazoea?

Kama Jobo kapeperushwa Kiushirikina ( Ndumba Nangai ) na Watanzania namwomba huyo Mganga au hao Waganga ili niwape Jukumu la Kuanza Kunifanyia Dawa kwa niaba ya Timu yangu pendwa Simba SC ili tarehe 8 May, 2021 nitoe Kipigo cha Shalubela ( cha Kikatili ) kwa Washamba wanaoenda Kufungwa na Azam FC Usiku huu wa Saa 2 na Robo kwa Mkapa.
 
Na huu ndipo ujinga wetu ulipo!
 
Mungu wetu kanunsuru tu na majanga yatupasa tumshukuru
 
Back
Top Bottom