Je,huu si ulaghai!?(utapeli)

Je,huu si ulaghai!?(utapeli)

Siri ya sifuri

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2018
Posts
2,335
Reaction score
1,967
Salaam wakuu.

Hii inakuaje!?

Pale unapounganishwa na huduma ya matangazo mtandaoni yenye malipo na ambayo hujaiomba,unakuta tu ujumbe umeingizwa kwenye Cm yako kwamba "umeunganishwa bure na huduma yetu kwa siku moja na baada ya hapo utatozwa shilingi 300 kwa siku.

Kujitoa piga namba 150.

Hivi ndivyo wabishi tunavyoendeshwa siku hizi,sasa basi angalau uuone na uusome huo ujumbe kisha wewe mwenyewe upuuzie kujitoa,lakini iwapo hujausoma na ukaufuta iwe kwa makusudi au kwa bahati mbaya, ndio tuseme utakuwa unatozwa hiyo pesa kila siku bila ya ridhaa yako na bila kujua!?

Wakuu wenye uelewa juu ya hii kadhia hebu tuelezeni namna inavyokuwa!.
 
Voda hao. Eti umejiunga na voda game. Utatozwa 300 kila siku. Li line lao sasa ni kwa ajili ya kupokelea simu tu. Ninaenda mwaka sasa sijaweka vocha wala kuweka pesa kwenye Mpesa.

Niliamua kujilipizia kisasi kwa kukopa na Wananidai nipige tafu na Mpawa wacha ile ya kukopa pesa ili kukamilisha mihamala.

Punbavu zao.
 
Heri ya wewe mkuu, umejua na kujihami mapema,wengine wanapigwa kimyakimya taarifa hawana!
 
Back
Top Bottom