GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
Utamkuta Waziri, Mkuu wa Mkoa na Wilaya pamoja na Watendaji wengine kila wakiwa wanatolea Ufafanuzi wa Jambo fulani wakiwa Wanahojiwa na Waandishi wa Habari ni lazima tu Watalazimisha kumtaja Rais wa Nchi (mfano wa sasa Samia) na hata kwa Wengine waliotuongoza Watanzania huko nyuma.
Hivi kwani Sisi Watanzania hatujui kuwa Rais wa Tanzania ni Samia Suluhu Hassan?
Na mnavyomtaja kila mara mkizungumza hata maeneo ambayo hamtakiwi Kumtaja ili Kuokoa muda huwa mnataka Kutuaminisha nini labda?
Kama kawaida yangu GENTAMYCINE ya kupenda Kutafiti na Kudadisi Jambo / Tukio nimejaribu kufuatilia Watendaji wa nchi za Ulaya, Marekani, South Africa, Uganda, Rwanda na Kenya wakiwa Wanaongea na Kutolea Ufafanuzi fulani wa Kiutendaji katika Serikali zao na hakuna mahala nimewasikia wakiwataja Marais wao na wala hawachukiwi na hao Marais kwa kutofanya Kwao hivyo.
Nikija kuwa Rais wa Tanzania nikiwa namsikia Mtendaji yoyote kila akiwa anaongea ananisifia au ananitajataja nitamuita Ikulu na Kumuwamba (Kumzaba) Vibao kwani nitajua huo ni Unafiki na Kujikomba kunakopitiliza Kwangu ili labda nami Nilewe Sifa na nisiwaze Kuwatumbua pale nikigundua Wameharibu mahala.
I hope Message Sent and Delivered!