ndio maana yake kama hataki ni kusema tu.
Kwa kweli ni mgeni kwenye safu hii ya JF, lakini naomba ushari.
Kuna msichana tulikubaliana kuoana, tumeshatambulishana na nimemchumbia tayari, kwa bahati nikapata safari ya ughaibuni hafla. tunawasiliana kwa sms au kumpigia mdamwengine. Tatizo nikimtumia sms za kuwa nampenda, namjali nafarijika kuwa nae lakini huwa hafurahii wala kunijibu kama na yeye ananipenda na badala yake hunitumia sms za kukatisha tamaa. lakini hajaniambia kuwa hanitaki. je nifanyeje?
Sasa na wewe acha kuwa unamtumia SMS ,mpigie simu za kawaida kumsalimia ..kama roho haijaanza kumuuma
Mkuu mnajuwa saa zingine na sisi wanaume tunakosea sana.....Kama unamuonyesha upendo na kumwambia maneno matamu kama hayo ila yeye hajibu then stop kusema hivyo kwa mda ongea nae kama dada yako alafu utakuja kuniambie mwenyewe........utaona tu amebadilika!!
uko sawa sana mkuu. Ni kumuuliza tu moja kwa moja uwe na uhakika. Kwa jinsi atakavyokujibu utapata picha tu hata kama hatakuambia moja kwa moja. Usimwogope sana kwa sababu ni mchumba wako na inabidi kuwa wazi sana.vunja ukimya. zungumza nae kuhusu hayo madai yako umsikilize atasemaje.