Je, Huyu Mkalimani Ramazani hajui kusoma? Kwanini aliweka dole gumba?

Je, Huyu Mkalimani Ramazani hajui kusoma? Kwanini aliweka dole gumba?

Duniahadaa

JF-Expert Member
Joined
Oct 16, 2017
Posts
336
Reaction score
677
Mangungo, Sultan wa Msovero katika Mwenyisagara, na Dk. Karl Peters. Mangungo sambamba na watu wake wote na Dk. Peters kwa niaba yake na washirika wake wengine wajao kwa pamoja wanaweka mkataba wa Urafiki wa Kudumu.

Mangungo amekubali kutoa himaya yake yote pamoja na watu wake na hadhi yake kwa Dk. Karl Peters, kama mwakilishi wa Chama cha Ukoloni wa Kijerumani (Society for German ya kuitwaa himaya yote ya Sultan Mangungo na haki zote kwa ajili ya Koloni la Ujerumani inayohusisha kila kona na amali za Mwenyi Sagara.

Katika kutekeleza hilo, Sultan Mangungo anakabidhi himaya yote ya Msovero, inayomilikiwa na yeye mwenyewe kwa urithi au kwa namna yoyote ile kwa nyakati zote, kwa Dk. Karl Peters, na wakati huo huo kumkabidhi haki zake zote.

Dk. Karl Peters kwa niaba ya Umoja wa Ukoloni wa Kijerumani anakusudia kuweka mkazo maalum kwa eneo la Msovero wakati wa kuitawala Usagara. Mkataba huu umewasilishwa kwa Sultan Mangungo na mkalimani Ramzan katika dhana ya wazi kabisa na umesainiwa na pande zote, kwa kuzingatia taratibu zilizopo katika Usagara, Sultan baada ya kuhojiwa moja kwa moja alikiri kwamba hakuwa na ushirika ama kutegemea kwa namna yoyote Sultan wa Zanzibar, na kwamba hakuwa hata akimfahamu.

Imesainiwa. Dk. KARL PETERS

Imesainiwa. MANGUNGO

Mkataba huu umefanyika kihalali kabisa na umehuishwa kwa nyakati zote mbele za mashahidi wengi, ambao tunakiri hapa:

Kwagakinga (dole gumba);

Golola mtoto wa Sultan Mangungo (dole gumba);

Draman mtoto wa pili wa Sultan Mangungo (dole gumba);

Graf Pfeil August Otto.

Dole gumba la mkalimani Ramazan

Dk. Karl Juhlke.

Msovero Usagara Novemba 29, 1884.
 
Hivi Msovero Usagara ni sehemu gani exactly hapa Tanzania? Ni mkoa gani? Wilaya gani?
 
Rais Samia hatoruhusu huo ubeberu, umepita kabisa! Let's pray for her health, life & extremely important responsibilities!
 
Ramazan namfananisha na dalali tu Kama hawa wa mjin anaipamba nyumba au chumba ili ukichukue kumbe nyumba ina shida kibao Kama kunguni malimbikizo ya luku ya nyuma ambayo unayalipa mpangaji bila kujua

So Rama alikuwa dalali ashachukua chake
 
Hile mikataba ilikuwa haina maana yoyote kwa waafrika. Kabla ya mkutano wa Berlin walitakiwa kuonyesha ni sehemu gani wajerumani, waingereza, webelgiji na wafaransa wamekubaliwa na watawala wa kiafrika kutawala. Na kuna sehemu walichonga mikataba ya uongo hili kuzuia wazungu wengine wasiingie katika maeneo hayo.
 
Nini tofauti Kati ya wakoloni na wawekezaji wa sasa
 
Back
Top Bottom