Je, huyu mtoto alitimiza muda wa kuzaliwa?

Mbwa dume

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2014
Posts
5,934
Reaction score
10,206
Habari zenu wandugu,

Ni muda mrefu nilikuwa kimya lakini yote ni katika harakati za utafutaji ukizingatia utawala huu hakuna tena zile dili za upigaji.

Niende kwenye mada,

Nina mdada ambaye niliwahi kuwa na mahusiano naye kipindi flani hivi then tukapotezana ikapelekea kila mtu kushika hamsini zake, kwani wazazi wake walihamia mkoa mwingine kikazi then polepole mawasiliano yakakatika.

Sasa tatizo ni kwamba mdada huyu alinijulisha kuwa kipindi naachana naye alikuwa na ujauzito japo hakujua, na hivi tunavyoongea tayari kajifungua mtoto wa kiume sasa hofu yangu inakuja hivi, nakumbuka tumeachana tarehe 16 January mwaka huu akiwa hana dalili za mimba.

Nakumbuka mara yake ya mwisho kuona damu ilikuwa December mwishoni na mpaka hiyo January tunaachana, nakumbuka kwenye tarehe 14 nilimpeleka hospital alikuwa akiumwa akapimwa vipimo vyote mpaka mimba hakuwa nayo isipokuwa walikuta tatizo la UTI ambapo alipewa dawa za kutumia na kufikia tarehe 16 January tukaagana akasafiri na wazazi wake na ndio ikawa mwisho kuonana kwetu zaidi ya mawasiliano kidogo kwa simu.

Mpaka hapa sina nia mbaya ya kumkataa mtoto ila hofu yangu ni kwamba, ikiwa mimba imeingia tarehe hizo alizoondoka yaani kati ya tarehe 15 na 16 January je inawezekana kweli ajifungue tarehe 5. Septemba?

Mbona ukihesabu miezi kuanzia ameondoka yaani tarehe 16.January mpaka tarehe 5. Septemba mbona miezi tisa haifiki? Ina maana huyu mtoto kazaliwa na miezi 8?na ikiwa ni hivyo je inawezekana mtoto kuzaliwa na miezi 8 akawa na hafya njema kama ilivyo kwa huyu?

Naamini humu jukwaani kuna wajuzi wa haya mambo pengine mimi sijui kuhesabu vizuri miezi.

Naomba kueleweshwa.

NB: Tarehe yake ya mwisho period =25/12/2016
Siku ya niliyompeleka hospital =14/01/2017 (vipimo vilionyesha hakuwa na mimba)
Siku aliyosafiri na ndio mwisho wetu kuonana 16/01/2017
Lakini amejifungua tarehe = 05/09/2017

Wadau naomba sana ushauri wenu kuhusu hesabu hizi maana mie naona miezi ya hiyo mimba haifiki 9!
 
Na huenda mkuu alizaliwa labda mtoto njiti huwezi kujua au kuna namna anataka akufanyie mchezo ubambikiziwe mtoto labda
 
Unataka ukatae ukiona ivyo!Mtoto n wako!inawezekana kabsa kuzaliwa kabla ya miezi Tisa.
 
Mtoto ni wako kabisa. Due date inaweza kuwe plus or minus 7 ya expected delivery date. Kwa hiyo tegemea kuwahi 5-9 days kutoka 16 ambaye au kuzidi kwa 7 days plus
 
Nimekusaidia kufanya pregnancy calculator inaonyesha angejifungua wiki ya 42 na Siku 2 ambapo ingekuwa 1st October 2017. Kwa hiyo amechelewa Siku 4 ambazo kitabibu ni kawaida. Hongera sana kwa kupata mtoto na mleee acha kulialia.
 
ni wako kbs !wemgine ile upt huwa inachelewa kuonesha km ana mimba !wengine huenda had mwez!huyo ni wako tafadhari mlee huyo mtoto !
 
Ulimtenda wakati anaumwa terehe unayotaja ni ya wewe kumpeleka hospital ambapo alikuwa hana mimba na ndio siku ya mwisho wenu weka sawa hapo tubadilishane mawazo ,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…