Je huyu mwanamke anafaa kuoa?

Je huyu mwanamke anafaa kuoa?

Mbwa dume

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2014
Posts
5,934
Reaction score
10,206
Binti huyu ameajiriwa kuuza duka la dada mmoja jirani na ofisini kwangu, anaonekana anajiheshimu na anaonekana mcha mungu, mimi binafsi nlishatendwa na niliyekuwa naye hivyo nimechoka na haya maisha ya kuwa mpweke nahitaji kuoa, baada ya kumchunguza binti huyu kwa miezi kadhaa nmetokea kuridhika nae, hivi sasa tuna mwezi mmoja tangu tuanze mahusiano.

Nikiwa najiandaa kwenda kwao nliamua kumuuliza kuhusu wazazi wake na maisha ya kwao kwa ujumla, binti huyu akiwa katika hali ya huzuni alianza kunisimulia historia yake kwa ufupi, ni mtoto wa nne katika familia ya watoto watano,mamake alifariki na kumuacha mdogo babake alikuwa anafanya kazi kwa wahindi na sasa kazeeka hana kitu, binti huyu amemaliza frm 4 na alijisomesha mwenyewe kwani familia ilisambaratika baadhi hawajulikani waliko,
akiwa masomoni aliwahi kukatisha masomo na kufanya kazi za ndani sehemu tofauti na aliwahi kubakwa na mwajiri wake, pia alifikia kujiuza ili apate pesa ya ada, aliwahi kubakwa na askari usiku,
alifanikiwa kumaliza form 4 na kupata cheti.
 
Kama ameamua kuweka maisha yake ya ndani wazi hivyo kwako jua amekupenda toka moyon. What if asingekuambia yote hayo? Kufunguka kwake kwako kunakupa mwanya mzuri zaid ya kutambua ni muwazi na amekupenda kwa dhati.
 
Matukio ya nyuma ya mpenzi wako yanaumuhimu wake!

Mshukuru Mungu kwa kupata ke mkweli but usisite kutafuta ukweli zaidi! Si unajua timing! Pengine kukuambia hivyo ili kuisaka ndoa tu!
Mtu hawezi kukuambia upuuzi wake! Na akiweza basi atakupa na grounds za kuhalalisha uovu huo!

Ndoa ni kupangilia mambo yaliyopo na kuforesee future!
...
Kuwa makini kijana!
 
binti huyu ameajiriwa kuuza duka la dada mmoja jirani na ofisini kwangu,
anaonekana anajiheshimu na anaonekana mcha mungu,
mimi binafsi nlishatendwa na niliyekuwa naye hivyo nimechoka na haya maisha ya kuwa mpweke nahitaji kuoa,
baada ya kumchunguza binti huyu kwa miezi kadhaa nmetokea kuridhika nae,
hivi sasa tuna mwezi mmoja tangu tuanze mahusiano.
Nikiwa najiandaa kwenda kwao nliamua kumuuliza kuhusu wazazi wake na maisha ya kwao kwa ujumla,
binti huyu akiwa ktk hali ya huzuni alianza kunisimulia historia yake kwa ufupi,
ni mtoto wa nne ktk familia ya watoto watano,mamake alifariki na kumuacha mdogo
babake alikuwa anafanya kazi kwa wahindi na sasa kazeeka hana kitu,
binti huyu amemaliza frm 4 na alijisomesha mwenyewe kwani familia ilisambaratika baadhi hawajulikani waliko,
akiwa masomoni aliwahi kukatisha masomo na kufanya kaz za ndani sehemu tofauti na aliwahi kubakwa na mwajiri wake,
pia alifikia kujiuza ili apate pesa ya ada,
aliwahi kubakwa na askari usiku,
alifanikiwa kumaliza frm 4 na kupata cheti.
Kama wewe ni risk taker, go ahead perhaps she might be something!
On the other hand Bundi ni Bundi tu!
 
Umesema umemchunguza na umeridhika naye sasa sijui unataka nini tena au sijaelewa? amekuambia alibakwa maanna yake si kwa hiari yake amejiuza ili apate kusoma na amepata cheti saiz umemkuta anauza dukani hiyo ni safari ya maisha yake yenye mabonde na milima ni muda sasa wa yeye kupata faraja ya maisha kama kweli unampenda msitiri mtoto wa watu ila usimpotezee muda kwa aliyoyapitia yanamtosha
 
anafaa sana,ukimuacha nipe mie,natafuta wa hivyo,anaejua maana halisi ya maisha.
 
anafaa kuwa mke kwa sababu na uhakika mpaka hapo anafanya mambo mke tayari
 
Ni wachache watafunguka kiasi hicho. Kama umeridhika na alivyo sasa endelea.
 
Back
Top Bottom