- Source #1
- View Source #1
Wakuu, naomba kuuliza. Huyu kweli ni mgombea wa kata ya Kilimani kupitia UDA? 🤔
- Tunachokijua
- Kenya inatarajia kufanya uchaguzi wake mkuu Agosti 10, 2027 ambapo viongozi mbalimbali watachaguliwa ikiwemo Rais, Wabunge na Magavana wa Kaunti.
Madai
Kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii kumekuwa na Poster inayomuonesha Hai Shi raia mwenye asili ya China na kutajwa kama mgombea wa kata ya Kilimani, Kaunti ya Nairobi kupitia chama cha United Democratic Alliance (UDA). Bango hilo limesambaa kupitia mitandao mbalimbali rejea hapa, hapa na hapa.
Uhalisia wa madai hayo
Baada ya ufuatiliaji imebainika kuwa Poster hiyo imehaririwa kutoka katika poster halisi na kubadilisha baadhi ya taarifa ikiwemo eneo, tarehe ya uchaguzi na nembo ya chama ili zifanane na za mchakato wa kuelekea uchaguzi mkuu unaoendelea nchini Kenya.
Poster halisi imebandikwa katika maeneo ya Afrika Kusini ambapo Hai Shi anagombea kupitia chama cha African National Congress. Hai Shi anagombea nafasi ya Udiwani katika kata ya 103 jijini Johernsburg.
Hivyo mgombea huyo ni Afrika kusini na si Kenya, anatokea chama cha ANC na siyo UDA, pia anagombea katia ya 103 na si Kilimani kama inavyodaiwa katika Poster iliyohaririwa.
Poster halisi