Mkuu ICC siyo kwa nchi za dunia ya tatu ingawaje hadi sasa mashitaka mengi yanayofanyiwa kazi ni ya nchi za dunia ya tatu. ICC tofauti na mahakama nyingine imeundwa kwa mkataba wa maafikiano baina ya nchi wanachama wa baraza kuu la umoja wa mataifa (UN General Assembly), ingawaje siyo chombo cha Umoja wa Mataifa. Baada ya Maafikiano hayo kuliundwa Rome Statute. Kila nchi ina uhuru wa kuamua kuafikiana na Rome Statute au la. Ninavyofahamu Marekani, Uchina na Urusi hawaafikiani au kwa maneno mengine hawaitambui ICC hivyo siyo rahisi kupeleka mashitaka kuhusu hizo nchi ICC. Kwa Marekani wakati wa utawala wa Clinton (mwaka 2000) alisaini Rome Statute, ila ilipofika mwaka 2002 utawala wa Bush ulifuta sahihi ya Marekani kwa Rome Statute (sijui kwa nini). ICC ina makosa maalum ambayo ina uwezo wa kuyafanyia kazi na vilevile uwezo wake wa kuendesha kesi una mipaka ndiyo maana kuna zaidi ya kesi 100 ambazo zimeshawasilishwa ila ambazo ina mamlaka ya kuzifanyia kazi siyo zaidi ya 20.