MwanaFalsafa1
JF-Expert Member
- Feb 26, 2008
- 5,565
- 843
Juzi hapa tulikuwa mimi na vijana wenzangu. As always vijana wakikaa maongezi mengi huanza. Ikaja topic ya HIV. Mtu mmoja akaniuliza je ukigundua msichana unayempenda sana ana HIV bado utamuoa au utasita? Jibu langu likikuwa sitoweza kumuacha na nitamuoa. Wenzangu wakaanza kusema kuwa nasema tu hivyo kwa sababu sijakutwa na kitu kama hicho. Swali langu ni kama nililo ulizwa mimi. Je ukigundua mpenzi wako ana virusi vya ukimwi bado utaendelea nae au utamuacha? Jibu langu mimi liko pale pale kuwa sitoweza kumuacha nimpendae kwa sababu ya virusi vya ukimwi.