MwanaFalsafa1
JF-Expert Member
- Feb 26, 2008
- 5,565
- 843
MwanaFA:
Kwa mausiano ya siku uwezekano mkubwa ni kuwa mtakuwa mmekwisha jamiiana naye. Kama ni hivyo, ni busara wote mkipima. Kama na wewe umeathirika kama yeye ni rahisi kuendelea na mahusiano yenu ingawa kutakuwa na kulaumiana mwanzo kuwa ni nani kati yenu kamwambukiza mwenzake.
Kama hujaathirika, ni busara ya kuangalia hali halisi. Tuko duniani kuishi bila kuweka risk yoyote. Sina uhakika mtu aliathirika anaweza kuishi miaka mingapi zaidi. Say miaka 20, then what happens there after? Je unamatarajio ya kuwa na watoto? Je mtaendelea kujamiiana? Kama ndiyo vipi kama kinga isipofanya kazi aslimia 100% can you take a risk?
Tahadhari kabla ya hatari lakini bila KUMSHUPAA muathirika yoyote.
Mhh..mkuu mwanafalsafa...maisha ni mafupi sana kuishi na risk around.....
First of all kama moja kati yenu akigundulika na HIV ambayo si AIDS.Kuna tatizo hapo ambalo ni la uaminifu..kwa statistis zinaonyesha ukiwa kwa kiwango kikubwa unaambukizwa kwa kufanya ngono.So upendo huo unao uzungumza wakati umetoka nje ukaupata...na unataka uendelee kupendwa..ohh no.Hii nazungumzika kwa male side.The same apply kwa mdada....kama ni mchumba wako..unacho weza ni kumpa support tu ya kimawazo..lakini no futher sex.Hii inakuweka safe sana rather than practise safe sex which is not 100% sure.
Life expentancy...mzee!! ni nini wataka kusema kuwa hata kama unaishi na mtu mzima huwezi jua atakufa lini kwa kuwa huna guarantee...hii haijastify...kuwa sasa uishi na mtu mwenye HIV.Let say hata unajua gari zima linaweza pata ajari...basi upande bovu?Fanya maamuzi ukiwa bado una nafasi ya kufanya maamuzi.Swali hili hili ukimuuliza mpenzi wako..u will get surprising answer....na mtazamo wako uta twist kiasi.
MwanaFA:
Kwa mausiano ya siku uwezekano mkubwa ni kuwa mtakuwa mmekwisha jamiiana naye. Kama ni hivyo, ni busara wote mkipima. .
Mw'FA,
Kwangu mm it will be over.
No way, sita muowa lkn uhusiano unaweza kuendelea wa kawaida tu.
Swali langu ni kama nililo ulizwa mimi. Je ukigundua mpenzi wako ana virusi vya ukimwi bado utaendelea nae au utamuacha?
Mkuu nimekuelewa. Kwanza mkuu tuchukulie kama mpenzi wako anao na wewe ukaonekana uko safe. Umeuliza je mtaishi miaka mingapi as in regard to life expectancy ya mpenzi wako. Ukatoa estimate ambayo ni 20 years which is just about right kama muathirika akifuata ushauri kwa makini. Lakini dies life expectancy matter? Hata ukimuoa asiye muathirika can you guarantee mtaishi wote zaidi ya miaka 20? Is it about the number of years you spend together or how you spend your time together?
Kuhusu watoto that's a medical issue which is complicated kidogo but it is possible. Ikibidi nita tafuta articles on that nikubandikie.
Kuhusu kinga. Mtu akiwa muathirika they must practice safe sex at all times. Japo hakuna kinga yoyote 100% but as long as you have safe sex chance ya kumuambukiza partner wako ni mdogo sana. It's the same risk as any other risk one encounters everyday as a virtue of being alive.
Mtu ukimpenda kwa dhati naamini utakuwa nae for better or for worse. Na pia you have to put yourself in the person's shoes. Je ungeathirika wewe na ukaachwa na mpenzi wako because of that ungeichukuliaje?
KIPI kinaanza.Ina maana watu wanaanza...kisha ndio wanaenda kupima?
Binafsi,ukweli wangu ni kuwa hata kama nikiwa nampenda mtu siwezi kuolewa nae huku ana HIV.
QUOTE]
Huu ndo ukweli na watu wengi wataamua kama wewe. Lengo la kuoana ni kujenga familia na mwisho kupata watoto. Sasa kama mmoja ana ngoma, itakuwa vipi?
Heri nusu shari haswa....
Ukijuwa nini lengo la ndoa, jibu lake litakuwa rahisi sana. Hapo kuendelea au kuto endelea kwa hiyo ndoa kutategemea sana na wewe binafsi nini unataka kwenye hiyo ndoa....wakikaa maongezi mengi huanza. Ikaja topic ya HIV. Mtu mmoja akaniuliza je ukigundua msichana unayempenda sana ana HIV bado utamuoa au utasita? Jibu langu likikuwa sitoweza kumuacha na nitamuoa. Wenzangu wakaanza kusema kuwa nasema tu hivyo kwa sababu sijakutwa na kitu kama hicho. Swali langu ni kama nililo ulizwa mimi. Je ukigundua mpenzi wako ana virusi vya ukimwi bado utaendelea nae au utamuacha? Jibu langu mimi liko pale pale kuwa sitoweza kumuacha nimpendae kwa sababu ya virusi vya ukimwi.
MwanaFA
Nitasema kweli kwani nitakuwa mpenzi wa MUNGU. Ingawa umeuliza kwa wanaume ila mimi kama mdada ikitokea imekuwa hivyo kwa mpenzi wangu nafikiri tutakaa na kulizungumza na nitamwambia wazi how I feel. Sitakuwa tayari kuendelea kuwa naye kimapenzi ila he will be the best friend ever. Nasema hili kwa sababu gani
1. Kuendelea naye au hata kuoana naye kunanimaanisha kujiweka katika risk (ambayo pengine nilijitahidi huko nyuma kujikinga!) kwa sababu suala la kujamiiana kwa kufuata maagizo sijui kutumia kinga (siliamini sana- what if ikaenda kombo siku moja?)
2. Kukubali kuolewa naye ni kukubali kuishi bila kupata watoto (dunia ya sasa kumwacha mtoto akiwa na umri mdogo bila ya wazazi ni dhambi kwa sababu jamii haiko kama ile ya zamani ambayo watoto walikuwa ni wa jamii na wala siyo wa MwanajamiiOne na mumewe tu)
3. Kujiweka kwako kwenye risk ni sawa na kuwakimbia na kuwanyima haki ndugu na wazazi wako ambao pengine wamekusomesha na kukukuza uje uwatunze sasa unapojiweka katika hali hii ina maana muda wako wa kuishi unaufupisha makusudi (ingawa unawezaishi zaidi)
4. Sipati picha pale ambapo ntakuwa nashughulika je mawzo yangu yatakuwa kwenye upendo wa kweli au ntakuwa nafikiria sijui leo nitaupata?
Kama muathirika ni mimi basi nitajitahidi kutokuwa selfish kama mwenzi wangu yuko safi nitampa ruhusa awe na mwingine aliye salama na nitampa option ya kuwa best friend kama atataka.
Si kwamba nanyanyapaa ila nimesema ukweli wangu (MSINIPIGE MAWE)