Je, inawezekana kuomba kutumiwa majibu ya vipimo kwa njia ya SMS?

Joined
Oct 5, 2015
Posts
60
Reaction score
3
Habarini wanaJF,

Naombeni kujua hivi inawezekana kwenda kupima HIV alafu majibu ukaomba utumiwe kwa njia ya sms yani usiyapokee hapohapo utumiwe kwa sms.
 
Ni makosa kufanya hivyo. Kabla ya kufanyiwa vipimo na kabla ya kupokea majibu yako unapaswa kufanyiwa counselling.

Kwani hiyo zinaa mlikuwa mkiifanya via Sms?
 
Habarini wanajf,naombeni kujua hivi inawezekana kwenda kupima HIV alafu majibu ukaomba utumiwe kwa njia ya sms yani usiyapokee hapohapo utumiwe kwa sms.

Ikimbieni zinaa maana inaua,jana umekuja na uzi wa "nina vinyama usoni,bado hukuridhika ukaja na uzi wa kaniambia nikapime damu,leo unatuambia utumiwe majibu za HIV Kwa sms,je sampuli ya damu nayo utaituma kwa sms?
 
Mariacluz umepoteza tumaini na nuru iliyokuwa machoni pako tangu utumiwe sms ukacheki damu yako ushauri wangu dada yangu jipe moyo uliomkuu na uamini wew ni mzima kabisa na hata ukikuta umeathirika ukimwi sio kifo dada angu kuna magonjwa ya kuogopa kama cancer ila sio ukimwi mtu anaishi na ukimwi 30yrs sasa unawezaje sema huu ni ugonjwa kuwa na imani nenda kapima mungu atakulinda ila kuwa muangalifu usije jidhuru kama unaona huna huo ujasiri nifuate pm kwa ushauri zaidi.be blessd dada
 
Ni makosa kufanya hivyo. Kabla ya kufanyiwa vipimo na kabla ya kupokea majibu yako unapaswa kufanyiwa counselling.

Kwani hiyo zinaa mlikuwa mkiifanya via Sms?

Kuna Hepatitis na Cancer na other terminal diseases. What's so special about HIV mpaka counselling iwe lazima ilhali almost everything one needs to know about it ipo everywhere?!
 
Ikimbieni zinaa maana inaua,jana umekuja na uzi wa "nina vinyama usoni,bado hukuridhika ukaja na uzi wa kaniambia nikapime damu,leo unatuambia utumiwe majibu za HIV Kwa sms,je sampuli ya damu nayo utaituma kwa sms?

Ahsanteeee Sana
 
Nashukuru sana kwa ushauri wako,ni wachache wenye kutoa ushauri wa kumfariji mtu as u did,but ukishapost hapa unakua tayari kupokea lolote sababu kila mtu anaandika analojisikia kuhusu post uliyoitoa..nakushukuru sana kwa ushauri wako na mungu akubariki.
 
Hapana hairuhusiwi, labda dozi ya ARV unaweza pewa maelekezo kwa
njia ya SMS ili usisahau namna ya kumeza.
 
jaman huyu dada mjibuni kwa upole tafadhali,nilisoma her previous story na inaonyesha kuwa bwana'ke alimcheat,so hata akipima akikutwa na ugonjwa(kwa mfano) itakuwa ciyo kupenda kwake....
 
Inawezekana. Njoo nikufanyie vipimo kisha nitakutumia majibu kwa sms. Au nikupatie Alere Determine ukajipime mwenyewe kwa muda wako.
 
ninahisi kuna mtu anashinikiza muende naye kupima... sasa kama we huna uhakika na afya yako fanya hivi, nenda peke yako hospitali yoyote bila kumpa taarifa ukapime (kama hujiamini tafuta mtu mwingine akusindikize)... ukipata majibu ndio urudi kwa huyo anayetaka muende naye huku ukijua kabisa majibu yatakuwaje.
 
Ni makosa kufanya hivyo. Kabla ya kufanyiwa vipimo na kabla ya kupokea majibu yako unapaswa kufanyiwa counselling.

Kwani hiyo zinaa mlikuwa mkiifanya via Sms?

kwani wote hupata ukimwi kwa zinaa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…