Je ingekuwa ni wewe ungeweza??

Je ingekuwa ni wewe ungeweza??

Edwin Chapa

Member
Joined
Jun 3, 2011
Posts
54
Reaction score
12
ANAKUFUMANIA: Analia, ananyamaza, anasononeka, unambembeleza anakuelewa anakusamehe halafu anasahau na anaendelea kukupenda!!!
...
UNAZAA NJE YA NDOA: Anasononeka na kulia sana. Anakuchukia lakini baadaye anakusamehe. Halafu analea mtoto uliyemzaa nje kwa upendo.
Kama ni kuchukiwa atachukiwa mtoto, si wewe uliyefanya umalaya!

UNARUDI USIKU WA MANANE UKIWA MTUNGI:Anakuwa na hofu kwa kuhofia usala...ma wako,Ukirudi anafurahi, Anakukaribisha vizuri, nakuandalia chakula, unagoma kula. Anahifadhi chakula alichokuandalia bila manung'uniko.

UNAAMKA ASUBUHI NA MAHANGOVER: Anakuandalia staftahi,supu n.k. (saa nyingine unagoma kutumia staftahi yake unakimbilia baa kwenda kunywa Supu na kuzimua. Wala halalamiki!

CHAKULA CHA USIKU: Ushapiga mtungi wako, unataka huduma. Unamrukia, hufanyi maandalizi yoyote unamuumiza.Ukishamaliza bila kujali kama mwenzako naye karidhika unageukia pembeni na kuanza kukoroma. Anavumilia ili akuridhishe. Na kesho yake tena inaweza tokea hii; hana kinyongo!

UNAJIANDAA KWENDA KIBARUANI: Unaamka,Unakuta tayari kakuandalia viwalo, suruwali imenyooshwa kama ya askari trafiki, shati limepigwa pasi ya maana! Nguo ulizovua jana zimeshalowekwa tayari kwa kufanyiwa usafi! Ulichomuudhi jana keshasahau na kukusamehe! anakutakia kazi njema kwa pendo!!!

UNAMPA UJAUZITO: Anauthamini, anautunza anajifungua kwa uchungu, mtoto anakuachia wewe umpe jina, la kwake halimo kabisa kwenye majina atakayotumia mtoto! Na pamoja na uchungu wa kuzaa, bado yuko radhi kukuzalia mtoto mwingine na mwingine tena! Na mengine meeeeengi sana wanafanyiwa hawa watu lakini

WANASAMEHE, WANAVUMILIA,WANAENDELEA KUTUPENDA! Kwa leo acheni tu niwape heshima zao wanawake wote:

LOVE WOMEN! GOD BLESS WOMEN!!!!!!"
 
natumia phone nimeshndwa kufanya editing

Sasa ya nini kuhamisha jukwaa moja kwenda jingine?

Ndugu, sio kila barua pepe au bandiko la Michuzi ni orijino - nyingi huwa zinaanzia humu barazani afu wadau wanazinyaka na wakiona ni madini, wana-paste na kusambaza.
 
Sijaelewa........................! ila kama tayari ilishawekwa humu haina ladha bro! labda kwa wale wasiokiona kama mimi.
 
Back
Top Bottom