Je Ingekuwaje.........What If...........??

Si vibaya kukumbuka and to cheris the good moments you once had together!
 
Reactions: Mbu
 


HATA MIMI YALINIKUTA Mwanajamii
 
aiseee.... i wish men would document this too
 
Maneno mengine wakati wa kutongozana huwa yanatamkwa kunogesha penzi tu, wala hayatoki moyoni. Kwa hiyo hata ukiyarekodi yanaweza yasisaidie sana kuamsha hisia upya pindi mapenzi yakishachuja! I am just thinking aloud!

Masaki nakubaliana na wewe. Kipindi hicho hata ukiambiwa thibitisha unayoyasema hata jana yake wakati mkiwa pamoja huwezi yathibitisha. Ni kuwa ahadi na mategemeo yanakuwa mengi na unajitahidi sana kutoa ahadi nyingi na matarajio pia yanakuwa mengi ila uhalisia unaufahamu mwenyewe huwezi fulfil kile ambacho unaahidi. Baada ya penzi kuchija ndo uhalisia wa muhusika unaonekana
 
Ukiniacha NTAKUUA.....Duh! hiyo karee....yaani huyo jamaa ni mkare si pore pore
 
ndo utajua binadamu mnafiki.especially wanaume.:ukiniacha sitaoa tena; kumbe mwezi ujao ana harusi
 
ndo utajua binadamu mnafiki.especially wanaume.:ukiniacha sitaoa tena; kumbe mwezi ujao ana harusi

Sasa Bebii nisiposema kile ambachop naweza sema muda huo unategemea nitakisema muda gani sasa. Uwongo sometime unasaidia katika kuhakikisha kuwa napata kile ninachokitaka na sio kila mahali unasema uwongo mwingine utakamatwa wakati utakapoulizwa kesho yake jana ulisema nini
 
haya bwana tushadanganyika tufanyeje sasa?
 
usigune bana haya ni mambo ya kawaida na yapo siku zote na wanaume tupo kama tumezaliwa na mama mmoja maana tunafanana kwenye fani sana
ni kweli wote moja jumlisha moja ni mbili
 

...tunapenda kusikia kile tupendacho kuambiwa. Wengine huomba hata wadanganywe wapate ahueni..!
Mapenzi ni Ugonjwa, kuna nyakati kudanganywa inageuka tiba.

Kuhusiana na mada hii, Ahadi na Viapo vya vyanzoni ni sawa na Cement na matofali wakati wa kujengea msingi
~ Love Foundation.

...hata msingi uwe imara kiasi gani, patatokea nyufa na mipasuko maishani.
Hakuna sababu ya kuhoji ubora wa Viapo na Ahadi mf; Cement ya Tanga, Mbeya au Wazo kwakuwa tu Nyumba inapitia misuko suko ya majira mbali mbali ya mwaka i.e Masika, kiangazi, kipupwe nk...i.e Seasons of Love

Kila nyumba (Ndoa) inahitaji matunzo na ukarabati (maboresho) ya hapa na pale kadri mnavyoendelea kukaa 'humo'
 

Na nyumba ambayo haina vitu kama hivyo kuna tatizo ndani ya nyumba husika
Tusiseme tuu kuwa hayo yalikuwa ni kwa ajili ya kumpata mhusika ila yalitakiwa kuwepo ili kulitilia mbolea penzi jipya na inapotokea mikwaruzano jua kwamba ni mapito na yalipaswa kuwepo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…