Je, ishu ya Adani kupewa kitengo cha makontena ndiyo iliyosababishwa Abdul Nondo atekwe?

Je, ishu ya Adani kupewa kitengo cha makontena ndiyo iliyosababishwa Abdul Nondo atekwe?

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
15,101
Reaction score
56,054
Connecting dots..

Kama kuna wanasiasa nchini walioisanua ishu ya ADANI kupewa kitengo cha makontena bandarini, basi ni Abdul Nondo. Wakati ule sisi tukiwa busy na ishu ya bandari (kubwa) waliyochukua DP World, huku nyuma serikali ya Bongo fasta fasta ilikuwa ikimsogeza ADANI Jikoni ili apewe kitengo cha makontena.

Sasa tunajua ADANI anamsala huko Marekani kutokana na mlungula mrefu anaodaiwa kutembeza. Wakati huohuo Kenya napo kimenuka, Serikali ya Kenya imefuta mkataba iliyokuwa imeingia na ADANI. Hapa bongo kelele dhidi ya ADANI zilikuwa zimeanza mdogomdogo. Na mwanasiasa ambaye angeifanya ishu ya ADANI kuwa ni turufu yake ni Abdul Nondo maana alianza na hii ishu kitambo sana.

Je Ishu ya ADANI imemponza Abdul Nondo?

Waliokula hela ya ADANI wanataka kumziba kijana mdomo?

Abdul Nondo ambaye ni member mwenzetu hapa JF amewahi kuandika makala kuhusu ADANI hapa:

Soma Yapi mahusiano ya Adani Group na TICTS huko Bandarini?
 
Hakika 'dot' zinaunganika vyema kwa upande wa huyu kijana; maana kwingineko sioni tatizo lolote naye kuihusu CCM kama chama na madaraka yake.

Huyu Adani kaingia kimya kimya sana bandarini. Zile kelele nyingi zilizo pigwa wakati wa DP World ndizo zilizo sababisha mambo mengine yote ya nchi hii yawe yanafanyika gizani.

Kwa mfano: Ni waTanzania wangapi wanao juwa kuwa Aani huyo kauziwa TICTS kwa $ 95 milioni. Kauziwa, siyo kuwa kakodiwa!
Hii ni mbali na PPP yake ya miaka 30 kwenye 'Container Terminal 2'!

Kwa mfano: Ni waTanzania wangai walio na ufahamu wa makubaliano Tanzania iliyo kubaliana na wa-Oman kuhusu ile gesi yetu ya Ntorya, kule Mtwara!
Hawa tume wakabidhi hawa watu kwa makubaliano yapi? Kuna anaye fahamu?

Kwa nini haya mambo yawe siri kubwa kiasi hiki?

Hizi nchi zilizo pata utajiri mkubwa kama hawa Oman, Qatar na kwingineko, kwa kutegemea mali asili zao, na wao walipata utajiri huo kwa kugawa mali asili zao kama tunavyo fanya sisi wakati huu?
 
Connecting dots..

Kama kuna wanasiasa nchini walioisanua ishu ya ADANI kupewa kitengo cha makontena bandarini, basi ni Abdul Nondo. Wakati ule sisi tukiwa busy na ishu ya bandari (kubwa) waliyochukua DP World, huku nyuma serikali ya Bongo fasta fasta ilikuwa ikimsogeza ADANI Jikoni ili apewe kitengo cha makontena.

Sasa tunajua ADANI anamsala huko Marekani kutokana na mlungula mrefu anaodaiwa kutembeza. Wakati huohuo Kenya napo kimenuka, Serikali ya Kenya imefuta mkataba iliyokuwa imeingia na ADANI. Hapa bongo kelele dhidi ya ADANI zilikuwa zimeanza mdogomdogo. Na mwanasiasa ambaye angeifanya ishu ya ADANI kuwa ni turufu yake ni Abdul Nondo maana alianza na hii ishu kitambo sana.

Je Ishu ya ADANI imemponza Abdul Nondo?

Waliokula hela ya ADANI wanataka kumziba kijana mdomo?

Abdul Nondo ambaye ni member mwenzetu hapa JF amewahi kuandika makala kuhusu ADANI hapa:

Soma Yapi mahusiano ya Adani Group na TICTS huko Bandarini?
Kwani yeye ndio adani?
 
Pia nondo alikuwa anaongelea sana juu ya ukosefu wa ajira kwa vijana. Connect dots na ukosefu wa ajira
 
Connecting dots..
Sasa marehemu Mzee Kibao, yeye 'dots' zake zinaangukia wapi; maana hadi leo nashindwa kuelewa kwa nini yule mzee alitendwa namna ile!
Sikuwahi kusoma makala yoyote aliyo andika juu ya jambo lolote, wala kusikia sauti yake kwenye jukwaa la siasa!
Yeye 'dots' zake zinakwenda vipi?
 
Nchi iko mikononi mwa genge dogo sana linalokula na kusaza. Linaweza hata kuua ilimradi usiguse masilhi yao ya kuibemenda nchi. Rasilimali za nchi zinaondoka kwa kasi ya ajabu. Yule bibi pale Ikulu anawaza kuendelea kuwa rais tu. Hilo kwake ndo lina maana zaidi. Hawazi rasilimali za nchi zitanufaishaje watu na vizazi vijavyo, yeye kanogewa na power tu baaasi. Kwake hilo ndo la muhimu zaidi.
 
Huyu Dogo Nondo ni moja ya vijana smart Sana katika nchi yetu.

Kipindi nyie mnapiga kelele za DP yeye aliona agusie na issue ya Aidan .

Tumebarikiwa kuwa na vijana wengi Ambao hawajitambui na ambao hawajui wanahitaji nini katika maisha yao.

Asante Sana Nondo
 
Back
Top Bottom