Pre GE2025 Je, itungwe Sheria mpya kuwalinda Wanawake dhidi ya Unyanyasaji kipindi cha Uchaguzi?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

figganigga

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
25,724
Reaction score
55,906
Salaam Wakuu,

Kwa mujibu wa Taasisi ya Kitaifa ya Kidemokrasia (NDI), katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020, wanawake waliochaguliwa kwa nafasi za ubunge ni asilimia 9.5, wabunge wa viti maalumu ni asilimia 29, hivyo kufanya jumla ya wabunge wanawake kuwa 142 kati ya 393.

Vilevile, ripoti ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ya mwaka 2020 inaonesha wanawake waliochaguliwa kwa nafasi za udiwani walikuwa asilimia 6.58 (260 kati ya madiwani 3,953), viti maalum walikuwa 1,374 katika halmashauri 184 sawa na asilimia 24.59. Kwa jumla, wanawake walikuwa asilimia 29.24 ya madiwani wote nchi nzima.

Ripoti ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Mwaka 2019 pia inaonesha kuwa kati ya nafasi 11,915 za wenyeviti wa vijiji, wanawake walishinda nafasi 246 sawa na asilimia 2.1, huku wanaume wakishika asilimia 97.9 ya nafasi hizo. Kati ya nafasi 4,171 za wenyeviti wa mitaa, wanawake walishinda nafasi 528 sawa na asilimia 12.6.

Kupata Taarifa na Matukio ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa kila mkoa ingia hapa:
LGE2024 - Special Thread: Orodha ya Mijadala ya Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 pamoja na Zanzibar

Idadi ya Wanawake wachache kujitokana inadaiwa ni sababu ya Udhalilishaji na unyanyasaji kipindi cha Uchaguzi kwa Wanawake ndo inawakatisha tamaa kushiriki siasa.

Udhalilishaji huo haufanywi kwenye Majukwaa tu bali udhalilishaji kwa wanawake unaofanyika hata mitandaoni unachangia kukatisha tamaa Wanawake kuingia katika ulingo wa siasa.

Ripoti ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Mwaka 2019 nayo inaonesha kuwa kati ya nafasi 11,915 za wenyeviti wa vijiji, wanawake walishinda nafasi 246 sawa na asilimia 2.1, huku wanaume wakishika asilimia 97.9 ya nafasi hizo. Kati ya nafasi 4,171 za wenyeviti wa mitaa, wanawake walishinda nafasi 528 sawa na asilimia 12.6.

Tafiti mbalimbali zinasema asilimia 75 ya Wanasiasa wanawake hawatumii mitandao ya kijamii kutokana na unyanyasaji wa kijinsia.

Hata hivyo Sheria nyingi zinawalinda Wanawake, nini kinafanya wasiende Mahakamani pale Wanaponyanyaswa na kidhalilishwa kwenye ulingo wa Siasa? Au Sheria hazijitoshelezi? Nini sababu kama ikiwezekena zitungwe Sheria mpya.

Kifungu cha 135 cha Sheria ya Kanuni za Adhabu, Sura 16, kinatambua unyanyasaji wa wanawake katika siasa kama kosa la uchaguzi.: "Mtu yeyote ambaye kwa makusudi ya kusababisha shambulio la kijinsia la aibu kwa kutoa maneno au sauti, kuonesha vitendo au kutoa maneno, au kuonesha ishara yoyote ambayo itaonekana na mtu mwingine atakuwa ametenda kosa la shambulio la kijinsia na akipatikana na hatia atawajibika na kifungo kisichozidi miaka mitano au faini isiyozidi laki tatu (Sh. 300,000) au vyote viwili.

Je, Sheria hii inaweza kuongeza idadi ya Wanawake wa kushiriki Maswala ya kisiasa au Sheria mpya itungwe yenye adhabu kali?
 
Hivi kwanini Tunamchukulia Mwanamke kama Ni kilema?

Yaani Kama Kuzaliwa Mwanamke basi ni ulemavu so inapaswa abandikwe Bango Kubwa Limeandika "HOLD WITH CARE"..

Kama aliamini anaweza Siasa na akachukua Form siasa Ina Mazuri yake na mabaya yake kama Mwanamke anaamini anaweza kufanya kama mwanaume kwanini Tumregard kama Special Groups..

Sasa Ile Equality Inayosemwa Kila Siku tuigeuze Iwe equity na Sio Equality???

Na kama Ni Equity vipi wanaofanya Hivyo hivyo kwa wanaume na wao pia Tuwalete majukwaani na tuanze kutetea wanaume pia?

Tunatengeneza Uoga Usio na Umuhimu na Tunatengeneza Ujasiri Fake...Sio Sawa
 
Back
Top Bottom