Je, jamii inawezaje kuyakabili magonjwa ya afya ya akili? ilinde afya yako ya akili, ni tunu yako

Je, jamii inawezaje kuyakabili magonjwa ya afya ya akili? ilinde afya yako ya akili, ni tunu yako

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Afya ya akili ni miongoni mwa mada zinazopuuzwa, zisizozungumzwa vya kutosha, pia zenye wataalamu wabobezi wachache sana kwa Tanzania. Lakini pia ni mada ngumu kuzungumzwa kutokana na kukosa uelewa sahihi kwa sababu jambo hili huchukuliwa juu juu pasipo upembuzi wa kina.

Mtaalamu mmoja wa masuala ya afya ya akili ambaye hakupenda kuandiwa jina lake, alisema, ’Wanaojita wataalamu wa afya ya akili wanashindwa kuishi kile wanachokifundisha au kukipigania kuhusu matatizo ya afya ya akili.”

Kutokuwa sawa kitaalamu upande wa afya ya akili kumesababisha matokeo ya uwepo wa magonjwa mengi ya akili katika maisha ya watu. Watu wengi wanasumbuliwa na magonjwa ya akili na utafiti unasema kadri siku zinavyoendelea ongezeko litakuwa kubwa.

Baadhi ya magonjwa ya akili yanayotesa watu wengi kimyakimya ni pamoja na haya yafuatayo. Mosi, mfadhaiko wa akili (depressionhapa baadhi ya watu hushindwa kutofautisha kati ya msongo wa mawazo (stress) na mfadhaiko wa akili (depression).

Tatizo la pili linalohangaisha watu ni ugonjwa wa wasiwasi au hofu iliyopitiliza (anxiety disorder),lakini tatu ni ugonjwa wa kupata mawazo ya kujidhuru/kujitoa uhai kwa sababu zozote zile. Magonjwa mengine yanayoathiri afya ya akili ni kubadilika badilika kwa hisia (bipolar disorder), kupoteza kumbukumbu (alzheimer’s disease), shida inayosababisha uwendawazimu (schizophrenia) pamoja na ugonjwa wa uongo (mythomania).

Magonjwa yanayoathiri afya ya akili yako mengi. Mengine ni hali ya mtu kutaka muda wote ajulikane au asikilizwe yeye tu, (histrionics personality disorder), tatizo la kiwewe yaani (post traumatic disorders) pamoja na matatizo ya kutojali au hali ya kutohurumia watu wengine (antisocial personality disorder). Haya ni baadhi tu ya magonjwa ambayo moja kwa moja huathiri akili.

Je, jamii inawezaje kuyakabili magonjwa ya afya ya akili?
Ni muhimu sana kuwaeleza watu Wanaokuzunguka namna unavyojisikia. Ni vema kuwashirikisha changamoto zako baadhi ya watu ambao nafsi yako inawaamini hasa katika kada ya afya ya akili. Elewa kwamba kutatua tatizo linaloweza kutibiwa kwa gharama ndogo ni muhimu kuliko kusubiri mambo yaende mrama.


Dkt. Naytham Masoud
Jarida la Fanaka
 
Mkuu Mimi Nina tatizo la Hofu iliyopitiliza yaani anxiety disorder sasa tunayaepuka vipi haya matatizo ya magonjwa ya afya ya akili . Ukinijibu hapa ni kwa faida ya wengine pia
 
Back
Top Bottom