Je, Kamanda Jumanne Muliro anatosha kuendelea kuwa RPC wa Dar?

Je, Kamanda Jumanne Muliro anatosha kuendelea kuwa RPC wa Dar?

Teko Modise

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2017
Posts
2,331
Reaction score
7,733
Kwa matukio yanayoendelea kila kona sasa ya mkoa huu, ni wazi kamanda Muliro kazi imemzidi na hatoshi kwenye majukumu yake.

Kila kona ya Dar ni matukio ya wizi tu mara panya road, mara vishandu, mali zetu zinakuwa rehani. Majira ya usiku kwasasa kama huna usafiri binafsi ni hatari sana kwa jiji hili.

Lakini cha kushangaza RPC Muliro yeye yuko bize kuhudhuria matukio ya mechi katika dimba la Lupaso, kila kukiwa na mechi camera za Azam TV lazima zituoneshe. Kamanda amka toka usingizini, uliletwa Dar kwa mbwembwe nyingi sasa chapa kazi, ile operesheni uliyoiendesha kule Chanika ihamie na maeneo mengine ya Dar.
 
Kaulize mwanza alichofanya muliro jumanne muliro huyo ni mtu wa vitendo sio muongeaji hao panya road wameingia cha kike.
 
Panyaroad ni watoto zenu wamalizeni wenyewe, hili la mtoto wa fulani taonekana mbaya, muolewe kabisa na panya road. Mnashindwa vipi kuvikalisha hivyo vitoto.
 
Kwa mfano tu tukianza na wewe mleta uzi usikute demu/wife wako tu anakushinda kumchunga unafikiri kuchunga mkoa mzima ni kazi rahisi? Kila mtu apewe muda kwa nafasi yake uhalifu haujawahi kuisha ila unapunguzwa
 
I wish I kud be RPC Watu wangezika mpaka wachoke, ni moto kwa kwenda mbele ilimradi tu tumethibitisha ww ni jambaz, mwizi, genge kama panya Road nk.

Wahalifu huwa wanaelewa risasi tu sio mahakama, ndio maana wanafungwa wakitoka wiki moja kafanya tukio tena.

Kwa waliokuwepo kipindi cha Tibaigana watakumbuka Dar ilikuwa haitawaliki, ni uporaji kwa kwenda mbele, alipoingia Kova mji ukawa baridiiii, ni chuma kwa kwenda mbele.

Muliro fanya kazi usisikilize sijui watetezi wa haki za binadamu kwenye wizi wakati wezi na wenyewe wanaua daily, piga chuma, tembeza shaba mwezi tu mji unapoa
 
Mbona hayo madogo?
Watu walipopugwa risasi mchana kweupe kule dodoma IGP hajajiuzulu.
Watu walitekwa na kupotea. Msikilize mdude n siro alikuwepo.
Akwilin aliuwawa na polisi wakafungwa kina mbowe . Sirro alikuwepo. Hajajiuzulu.
Ni mengi na yanaumiza sana! Itoshe tu kusema hajajiuzulu kwa sababu ana kadi ya ccm
 
Back
Top Bottom