Je, kanisa la mhubiri Christopher Mwakasege liko wapi?

Hizi siku za mwisho ngumu sana kujua who is who, afu hawa wachungaji mbona huku sumbawanga vijijini hawaji? Mwanza,arusha, dar jmn dhambi zikl na huku
 
mkuu kwa ushauri wa bure kati ya mambo unayopaswa kuchunga ni kumsema mtu hasa mtumishi wa Mungu ambaye wewe huna ushaidi wa tuhuma hizo yatakukuta makuu msaada uupate kwake huyo huyo unayemsema. Usicheze na Mungu!
Kipi kinachokusadikisha ni watumishi wa Mungu? Kutumia Biblia ambayo hata hivyo wanaitafsiri kiaina aina? Kufanya mazingaombwe mawili, matatu hata mia ambayo baada ya muda mambo hurejea kama kawaida? Au makoti na tai ndefundefu, magauni na vilemba vya bei mbaya na perfume wanazonunua kwa ngawira zenu?
Ndugu yangu unajijengea hofu ya bure; kwani hao hawana kibali toka kwa Mungu bali ibilisi anayezurura hapa duniani kuharibu kazi za watu.
Kama kweli wahuni hao wana uwezo wa kuwaombea wagonjwa na wenye shida na kuwaponya kwa jina la "Yesu" (ingawa si Yesu wa kweli anayafanya kazi ndani yao) mbona hawaendi Bugandi, Ocean Road, Muhimbili, KCMC, Lugalo na kwingine ili wawaombee na kuwaponya wote wanaohangaika na kuteseka huko na Hospitali kubaki wazi?
Yesu alisema "Mtawatambua kwa matendo yao" na ni kweli wanatambulika maana chema chajiuza, kibaya chajinadi na kujitembeza.
Kwao unapata uzushi, fitina, kupoteza mali na fedha, ulaghai, vitisho, uongo, kujikweza, usengenyi na kila aina ya uchafu!
Ni watoto wa ibilisi walio kazini kwa jina la Yesu. Alikwisha onya kwamba watakuja, wataponya, watafanya "miujiza" na kuhubiri kwa jina lake ingawa hatakuwa amewatuma! ukitakachukua ukweli huu au uuache.
 
Tangu lini kanisa likamilikiwa na mtu binafsi?? Rwakatare,Gwajima,Lusekelo,Malisa,Kakobe,Gamanywa, na walokole wengine wanamiliki makanisa kitu ambacho ni ubatili na bible imetuonya.Wanatumia nguvu za giza kama wafanyavyo waganga wa kienyeji kutuliza mapepo.Jina la Yesu wanalitumia kwa uzushi huku wakifanya mambo ya uganga makanisani.Mwakasege na mke wake ni matapeli bingwa kwa kutumia mapepo katika miujiza yao ya uongo.Manabii wa uongo hawa.
 
Inahitajika roho ya kiinjilisti kurusha jambo la kiinjili humu. Nimesoma kimya kimya mwishowe nikaona bora niseme neno.
A piece of advice: usijaribu kumtetea mtu ambaye ambaye Mungu wake yuko hai.
Wewe dada imeandikwa watakuja manabii wa uongo nao watadanganya wengi yumkini hata wateule.watafanya maajabu ya uongo.
 


Mkuu we ndo umemaliza kila kitu kabisa. Ni kweli sijawahi kusikia hao matapeli hata mmoja akienda si zahanati wala hospitali yeyote ile kuwaombea wagonjwa wanaoteseka.

Ni kanisani na kwenye matamasha viwanjani, wakishamaliza wanakuambia toa kwa jina la bwana ubarikiwe.

Nafanya mpango nikute na mchungaji mmoja aliyebadili dini na anielezee wanafanyaje kupumbaza waumini wake hadi inakuwa vile huku wakitoa Sadaka bila mapenzi yao binafsi bali kwa miujiza wanayofanya. Na ipo njia ya kufanya il umshtukie ujanja wake wakati wanapojifanya kumuombea mgonjwa na wengine ni wagonjwa fake huandaliwa kabisa.

Huyo X-mchungaji kwa sasa yupo Mbeya ila kuna mmoja nae jina limenitoka ameshatoa sana video za kuonyesha uovu wanaofanya ni mtu wa Songea na baba yake ni Mchungaji huku akitangaza katika Radio flani hivi ya dini(Unaweza kumtafuta) yeye kamwaga kila kitu. Na mchungaji mwingine aliyebadili dini huku akitoa siri za hao matapeli walishamuua kimafia ni Iman Petro (R.I.P)
 

Ni vema sana kuepuka kusema kwa ujasiri kitu ambacho kina husisha imani. Kama wewe usivyoamini kuwa kuna watumishi wa MUNGU, wapo wanaoamini kuwa wapo. So hii ni mitazamo miwili tofauti ambayo hakuna mwenye haki ya kusema kuwa yeye yuko sahihi kuliko mwingine kwa sababu ni masuala yahusuyo imani ya mtu. Jaribu kujitahidi kumconvince mtu aikubali imani yako kwa hoja na sio kashfa. ... umeuliza kipi kinasadikisha waamini kuwa ni watu wa MUNGU, wewe ni kii kinachokufanya usiamini kuwa ni watumishi wa MUNGU?................................................Suala la kwa nini wasiende kuombea wagonjwa wa mahospitalini bado ni suala la imani, hata hao wanaokwenda kuombewa huko kwenye mikutano sio wote wanaoponywa, ni kutokana na imani zao. Kama mtu hana imani kuwa yupo mwenye nguvu na uweza hata akiombewa akamwagiwa maji pipa hatopona. Na mwisho kumbuka anayeponyesha ni MUNGU na wala sio hawa watumishi wake ambao ni binadamu tu kama sisi. ILA nakubaliana na wewe kuwa wapo watumishi ambao si wa kweli maana hata katika vitabu vitukufu tumeaswa juu yao.
 

umekomaa kusema si watumishi wa Mungu ila hujaweka wazi wapi ndio watumish. Kwani hujui hata Yesu alipokuwa duniani katika mwili hakuponya kila mgonjwa ila wale waliokuwa na haja, au unataka kujitoa ufahamu kuwa hata kipindi cha Elisha kulikuwa na wenye ukoma wengi ktk Israel na aliyeponywa alikuwa Naaman ambaye si Mwisrael? Au umesahau pia wakati wa Eliya kulikuwa na wajane wengi ila muujiza wa chakula ulifanyika kwa mama mjane wa Serepta tu? Je umesahau kuwa pia Yesu alipokuwa duniani hakufufua kila mtu ila watu watatu tu?
Ok unasema wanataka pesa umesahau pia kanisa la kwanza liliuuza kila kitu kwa ajili ya Injili?(matendo 4:32-37)
Kama hujui Mungu akurehemu, ila kama unajua WEWE NI AGENT WA MPINGA KRISTO.
 

mkuu umejibu vyema sana, nimewauliza maswali hawa ndg ktk post zangu wamejifanya kama hawajaziona. Na hata ulichowauliza hawatajibu ila kupinga tu.
 
Mnarumbana nini? serikali ya mtu ni kichwa chake na rais wa mtu ni pesa yake. Asiyeamini kivyake vyake, anayeamini amekwisha kuokolewa, hayo si maneno yangu.
 
naona wengi wenu hamna ufahamu na maarifa. huwezi kuongelea uongo. bila kusema ukweli ni upi
 

We kama unaamini ni ibilisi kaa hivyo hivyo, anaeamini ni mtumishi wa mungu basi mwache aamini! We ni nani hata useme uliyosema? na kwa uzoefu tu we ni mwislam jaribu kuheshim iman za watu.
 

dah mkuu wewe ni hatari! nisingependa kuleta mabishano ya bure ila napenda kusema tu watu wa aina yako walikuwepo tangu enzi za Yesu, hata wengine walimdhiaki wakisema kama kweli wewe ni mwana wa Mungu fanya hivi hata ibilisi alisema hivyo hivyo! haina tofauti na unachokisema ndugu yangu kuwa kama kweli wao ni watumishi waende mahospitali! ila maandiko yanasema siku za mwisho watakuja wenye kudhiaki! angalia wewe usiwe mumojawapo wa kutimiza unabii wa biblia!
 
We kama unaamini ni ibilisi kaa hivyo hivyo, anaeamini ni mtumishi wa mungu basi mwache aamini! We ni nani hata useme uliyosema? na kwa uzoefu tu we ni mwislam jaribu kuheshim iman za watu.

yani ni kweli mkuu siwezi amini huyu jamaa atakuwa ni Mkristo achilia mbali aliyeamini! lazima hii ni roho nyingine
 

Dah huyu si voice of wisdom bali Roho wa Bwana yu ndani yake! AMEN
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…