Hapana ilikuwa kabla ya hilo ni wakati wa mahubiri ya jangwani. Mwakasege anaijua vizuri bible so anaona akichomekea maombi ya pesa kupitia hiyo atapata na kweli anapata. Atakapobadilika arudi kufundisha watu neno la Mungu ili waache mabaya ndipo nitamrejelea tena.
Kama u mfuasi wake nazidi kumchukia mwakasege pia.
Vijijini hamna miundo mbinu.....Mbona huwa haendi vijijini?
unajua mtu akiwa tu anaunganisha matukio ya mambo ya fedha tu anaonekana yeye ni Mgalatia,jamani dunia imebadilika sana sana,lazima injili iunganishwe na fedha,kuwa na fedha sio dhambi,dhambi ni umezipataje,na unazitumiaje,Injili bila fedha haiendiiiii.Najua mtanichana. pamoja na kuwa mwakasege ni mlutheri mwenzangu mi simkubali kabisa toka alipoingiza somo la uchumi kwenye mahubiri yake. Before he was good. alipoijua shilingi mmmmh.
Bado tu mnataka kwenda kuliwa hela zenu na wajanja wakaendeshee Hummer?
Ama kweli bora uwe maskini kihali lakini usiwe maskini wa kujitambua kifikra.
Ole wao wamdhiakio roho wa Mungu.Mwaksege ni mtumishi wa Mungu tena mpakwa mafuta wake na mpendwa katika wapendwa wake ndugu
nasikia jamaa ni freemaso
Hata mimi namkubali Mwl. Mwakasege lakini huwa simwelewi anapofanya huduma mara nyingi mikoa ya Arusha, Dsm,Dom & Mwanza zaidi ya mara moja kwa mwaka na kila semina huchukua siku 7. Lakini mikoa kama Kigoma, Shinyanga, nk. anafanya semina mara moja kwa mwaka halafu inakuwa ya siku 3.Mwalimu Mwakasege yuko juu sana huwezi kumlinganisha na watumishi wengi kwasababu moja kubwa,hafungwi na minyororo ya madhehebu.Nimewahi kuhudhuria semina nyingi za Bwana Mwakasege sikuwahi kumsikia hata siku moja akiwaelekeza watu waende kwenye dhehebu fulani fulani.
Kuna kasoro moja kubwa ambayo nimeiona kwa Bwana Mwakasege siku za karibuni amejikita sana kuwahimiza watu kwenda Israel.Amefikia hatua ya kuandaa safari za kwenda Israel kwa wanandoa as if uponyaji unapatikana unapokwenda Israel.Bwana mwakasege ndiye aliyemshauri E Ngoyai Elowassa kwenda Israel mara baada ya kuitia hasara kubwa nchi yetu na mkataba wa RICHMOND badala ya kumshauri aombe radhi watanzania kwa uzembe anamshauri aende Israel.
naomba web yake, kama unaijua, kuna wakati nilikua naitumia lakini ikafika mahali ikagoma kufungua....
Ni nani anayemjua vyema huyu ndugu?
Nasikia ni Mhubiri,
je kanisa lake liko wapi?
Christopher Mwakasege is a true servant of God. Mtawatambua kwa matunda yao. Matunda yake kwa muonekano na kwa malisho ni upendo, uvumilivu, utu wema, upole, kiasi, fadhili, unyenyekevu,amani na uaminifu.
Sasa kama haya yote tunayaona kwa mtu si ndio tunda la roho hilo, kwani tangu lini mbuyu ukazaa maembe?
Hizi siku za mwisho ngumu sana kujua who is who, afu hawa wachungaji mbona huku sumbawanga vijijini hawaji? Mwanza,arusha, dar jmn dhambi zikl na huku