Je, kanisa la mhubiri Christopher Mwakasege liko wapi?

Mwalim christopher mwakasege,
nashukuru nimerudi JF kupata kile nilicho taka kujua kupitia google
 
Ni nani anayemjua vyema huyu ndugu?
Nasikia ni Mhubiri,
je kanisa lake liko wapi?

Kweli bujibuji unamapepo. Huyu jamaa ndio mchungaji pekee wa ukweli, hana kanisa wala wafuasi, anafundisha uchumi ile mbaya, nasikia ndio alikuwa mshauri wa rais wa mambo ya uchumi enzi za utawala wa Mwinyi
 
mimi kidogo namfahamu mwakasege
Ni mnyakusa wa Tukuyu baba wa watoto wanne 3 wasichana na 1 mvulana na ni mme wa mke mmoja. Ni mtaalamu wa uchumi na mipango aliysoma chuo kikuu cha Dar. Alianza kazi kama afisa mipango ktk wilaya ya Arumeru akiishi ktk nyumba za carmatec Duluti, baadaye aliacha kazi serikalini na kujiunga na KKT makao makuu kama afisa mipango na uchumi. Miaka ya tisini alianza kufundisha mafundisho hayo ya kiroho. Kumbuka yeye ni MWALIMU sio nabii wala mchungaji, baadaye aliacha kazi KKT na kujihusisha na shughuli binafsi alifungua ofisi yake inayoitwa TASOET inayojihusisha na ushauri wa uchumi na mipango pia serikali ya awamu ya tatu kampuni hii ilikuwa miongoni mwa kampuni zilizohusika na Debt advocacy ili serikali ipunguziwe madeni. Pia amekuwa akijihusisha na uandishi wa vitabu vidogo vidogo vya mafundisho ya kiroho cha kwanza kikiwa ''Jifunze kusamehe na kusahau'' pia amekuwa akichapiza vigazeti vinavyoitwa MANA kula ukue kiroho, pamoja na uuzaji wa audio na video tapes za mahubiri yake. Amekuwa akiandaaa mikutano yake kupitia timu huru ya NEW LIFE CRUSADE COMETTEE ni timu huru kwa sababu ina wanakamati toka madhahebu yote ya kikristo ktk mikoa yote ambayo anafanya semina, mbali na maombezi semina zake zinahusu ukuaji wa kiroho na jinsi ya kuishi kama mkristo. Pia amekuwa akiandaa safari za Israel ''visit to the holy land'' pamoja na marriage retreat hukohuko. Yeye sio mchungaji na hana kanisa wala dhehebu ni muumini wa kanisa la KKKT kanisa la kijenge. Kwa sasa anaishi Njiro Redio. Hivyo ni kwa ufupi jinsi mimi nnavyomfahamu, mwalimu Christopher Mwakasege
 

pukudu umesema kweli
 

:help::kev:
 
yah: Christopher Mwakasege

Mtumishi mwakasege ni kweli ameitwa na Bwana kwa utendaji wa kazi yake na mungu amekupa vitu vizuri vya kuwajenga watu katika imani na mara nyingi nimesoma masomo ya kwenye website yako mfano Roho Mtakatifu, Damu ya Yesu jinsi inavyoweza kulate upatanisho na katika maombi niliamua kufanyia kazi kweli nilipata kitu cha tofauti nanikajiona inavyotenda kazi damu ya Yesu kusema kweli ninayafurahia mafundisho na huwa napenda kila wakati kusoma. kuna somo moja linahusu habari ya kusamehe kwakweli lilinifungua sana na mpaka nilijikuta na mimi nilienda kuwafundisha wenzangu habari ya kusamehe na kupitia hivyo Mungu aliwafungua watu maana walikuwa hawajajua ni maana ya kusaheme na kama hujasamehe kuna hasara gani kubwa. mimi na sema Mungu ambariki sana na azidi kumuinua zaidi na zaidi.
 
yah: Christopher Mwakasege <BR><BR>Mtumishi mwakasege ni kweli ameitwa na Bwana kwa utendaji wa kazi yake na mungu amekupa vitu vizuri vya kuwajenga watu katika imani&nbsp; na mara nyingi nimesoma masomo ya kwenye website yako mfano Roho Mtakatifu, Damu ya Yesu jinsi inavyoweza kulate upatanisho na katika maombi niliamua kufanyia kazi kweli nilipata kitu cha tofauti nanikajiona inavyotenda kazi damu ya Yesu kusema kweli ninayafurahia mafundisho na huwa napenda kila wakati kusoma.&nbsp; kuna somo moja linahusu habari ya kusamehe kwakweli lilinifungua sana na mpaka nilijikuta na mimi nilienda kuwafundisha wenzangu habari ya kusamehe na kupitia hivyo Mungu aliwafungua watu maana walikuwa hawajajua ni maana ya kusaheme na kama hujasamehe kuna hasara gani kubwa. mimi na sema Mungu ambariki sana na azidi kumuinua zaidi na zaidi.
 
namshukuru aliyeanzisha hii topic.namkumbuka mwakasege alisoma iyunga sec --mbeya 1972--1975.baada ya hapo sikujua alielekea wapi mpaka nilipomuona kwenye tv akihubili.
 


Sijaona kosa la Mwakasege kushawishi watu kwenda Israel. Kwetu Wakristo Israel ni sehemu ya kwenda Hijja kama ilivyo kwa Waislam kwenda Makka. Unaposema kuwa hiyo ni kasoro ya Mwakasege ina maana unamaanisha hata Waislamu kushawishiwa kwenda Makka ni makosa
 
Huyu ni mbabaishaji tu anaepata kula yake kupitia migongo ya waliokata tamaa. Hana tofauti na kina Anthony Lusekelo na wengineo. Asanteni!
 
Huyu ameitwa kweli kweli na Mungu yupo juu yaani jina la Bwana libarikiwe sana tuzidi kumwombea tu naombeni website yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…