John Magongwe
Member
- Jan 4, 2024
- 71
- 119
Je Kanisa la Sasa ni Moto au ni Vuguvugu kama Kanisa la Laodikia ?
Kanisa la Laodikia ni nini
Kwanza hebu tujikumbushe historia ya yale makanisa saba, tunayoyasoma katika kitabu cha Ufunuo, Aya ya 2 na ya 3. Makanisa saba tunayoyasoma katika kitabu cha Ufunuo ni makanisa ambayo yalikuwa katika miji 7 tofauti tofauti. Miji hiyo ni Efeso, Smirna, Pergano, Thiatira, Sardi, Filadelfia na Laodikia (Ufunuo 1:11). Kila kanisa lilikuwa na tabia yake.
Kanisa la Efeso lilikuwa limeacha upendo wake wa kwanza. Kanisa la Smirna lilipitia mateso. Kanisa la Pergano lilihitaji kutubu. Kanisa la Thiatira lilikuwa na nabii wa uwongo. Kanisa la Sardi lilikuwa limelala. Kanisa la Filadelfia lilikuwa na uvumilivu. Kanisa la Laodikia lilikuwa na imani isiyo baridi wala isiyo moto.
Makanisa hayo yalijulikana kwa majina ya miji hiyo, na miji yote ilikuwa inapatikana katika eneo lijulikanalo kama Asia Ndogo, ambalo kwa sasa ni nchi ya Uturuki.
Kati ya makanisa saba yaliyoandikiwa na Mtume Yohana kwa ajili ya kuyaimarisha, kanisa la Laodikia ndilo lilikuwa la saba na la mwisho kuandikiwa barua.
Jumuiya za makanisa hayo saba huko Uturuki, ni mfano wa kanisa lote duniani kote.
Tabia za kanisa la Laodikia katika biblia
Ufunuo 3:14 “Na kwa malaika wa kanisa lililoko Laodikia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye Amina, Shahidi aliye mwaminifu na wa kweli, mwanzo wa kuumba kwa Mungu.
15 Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto. 16 Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu. 17 Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi”.
Hizo ndizo zilikuwa tabia za kanisa la Laodikia. Kati ya yale makanisa saba, ndilo lilikuwa kanisa la saba. Biblia inasema ni kanisa ambalo lilikuwa vuguvugu, si moto wala si baridi.
Katika baadhi ya makanisa ya wakati huu, utaona mtu mguu mmoja nje, mguu mmoja ndani, leo yupo kanisani kesho disko, leo anamwabudu Bwana kesho anasikiliza miziki ya kidunia, simu yake nusu ina nyimbo za injili nusu nyimbo za kidunia, kabati lake nusu lina nguo za kujisitiri nusu lina nguo za nusu uchi, maneno yake nusu ya heshima nusu ya kihuni, biashara yake nusu ni halali nusu ni haramu, duka lake nusu lina bidhaa njema nusu lina bidhaa haramu, leo atatoa sadaka kesho anahonga au anahongwa, n.k
Hiyo ndiyo ilikuwa hali ya kanisa la Laodikia na ndiyo hali ya baadhi ya makanisa yaliyopo.
Tangu zamani, shetani amekuwa akibuni njia mbali mbali za kumfanya mwanadamu aangamie kwa anguko litakalomfanya asiweze tena kurudi nyuma. Na amekuwa akifanya hivyo kwa kuchunguza ni njia ipi inayomchukiza Mungu zaidi kuliko nyingine. Na akishaipata anakwenda kuwashawishi wanadamu waitende hiyo, ili Mungu asiwe na huruma kwao, waangamizwe moja kwa moja.
Kwa mfano, tukisoma katika agano la kale, Bwana aliwapa wana wa Israeli amri 10, na zile nne za kwanza, zilimuhusu Mungu mwenyewe. Waliambiwa wasiwe na miungu mingine ila Mungu wa Israeli, waliambiwa pia wasijifanyie sanamu ya kuchonga, kwani yeye ni Mungu mwenye wivu, waliambiwa pia wasilitaje bure jina la Bwana Mungu wao.
Sasa ukichunguza, utaona shetani alipoona kuwa hizi ndizo Mungu kazitilia msisitizo, na kaziwekwa za kwanza kabisa, tena alipogundua kuwa Mungu ni Mungu mwenye wivu, ndipo akaanza kuwekeza nguvu zake zote hapo. Yaani kuwashawishi watu waiendee miungu mingine, na kuabudu sanamu, ili tu, Mungu atiwe wivu, awateketeze watu wake kwa maangamizi yasiyoweza kuponyeka, Na ndiyo maana ukisoma agano la kale, makosa mengi yaliyokuwa yanawakosesha wana wa Israeli wakati wote mpaka kuwasababishia kupelekwa utumwani, ni ibada za sanamu.
Hiyo ndiyo imekuwa desturi ya shetani katika vizazi vyote, lakini pia katika kipindi hichi tunachoishi. Mungu alitoa amri ya kile anachokichukia zaidi na ndipo hapo hapo shetani naye akaenda kuwekeza zaidi nguvu zake ili awaangamize watu wengi kirahisi.
Hivyo, ni wajibu wa kila mmoja kufahamu kuwa tunaishi katika kanisa la mwisho la LAODIKIA, kulingana na unabii wa kibiblia. Kumbuka yalikuwepo makanisa mengine sita, nayo yalishapita na jumbe zao, na sasa tupo katika kanisa la mwisho, na litaishia na unyakuo. Yaani, kanisa la saba la Laodikia linawakilisha kanisa lote kabla ya ujio wa Yesu mara pili. Tupo katika kipindi hicho cha kabla ya unyakuo.
Katika hili, kanisa la 7 ambalo ndilo tunaishi mimi na wewe, Mungu alizungumza na sisi na kutugawia amri ambayo inapaswa isivunjwe, kama tu ile amri ya kwanza ilivyokuwa katika agano la kale, kwamba mtu yeyote asiwe na miungu mingine ila yeye. Kadhalika na katika kanisa hili la mwisho, Bwana alitoa amri, akasema uwe moto. Akaongezea pia na kusema kama huwezi kuwa moto, ni afadhali uwe baridi. Hakuishia hapo, akaelezea jambo analolichukia kuliko yote, nalo ni kuwa vuguvugu (Ufunuo 3:15-16).
Shetani kwa kulijua hilo, ili amwangamize mwanadamu vizuri, na kumvunja vunja kabisa, alikwenda kuwekeza nguvu zake zote mahali ambapo panamkasirisha Mungu zaidi, ili tu mwanadamu atakaponaswa hapo, iwe ni vigumu kupona, aangamie milele, na sehemu hiyo siyo nyingine, bali ni kumfanya mtu awe vuguvugu.
Shetani anachofanya yeye sasa na majeshi yake, ni kuhakikisha kwa nguvu zote watu wanakuwa VUGUVUGU. Yaani, anahakikisha kuwa mtu anamfahamu Mungu, lakini amchanganye kidogo na mambo ya giza. Anafanya juu chini mtu aende kanisani, baadaye akitoka aende disko. Hataki awe ni mtu wa disko tu siku zote na asiende kanisani kabisa hata siku moja. Hataki mtu awe ni wa kidunia tu siku zote na hata siku moja hana habari na Mungu. Anataka vyote vifanyike kwa pamoja, kwa sababu anajua Mungu amesema ni heri mtu awe baridi kabisa kuliko VUGUVUGU.
Bwana Yesu alisema maneno haya kwa kanisa hili:
Ufunuo 3:14 “Na kwa malaika wa kanisa lililoko Laodikia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye Amina, Shahidi aliye mwaminifu na wa kweli, mwanzo wa kuumba kwa Mungu. 15 Nayajua matendo yako, YA KUWA HU BARIDI, WALA HU MOTO; ingekuwa HERI kama ungekuwa baridi au moto16 Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, NITAKUTAPIKA UTOKE KATIKA KINYWA CHANGU”.
Ili shetani afanikishe jambo hilo, aliwatia mafuta watumishi wake, kuwafanya watu wawe BARIDI, pamoja na kuwa VUGUVUGU. Wale wanaowafanya watu wawe baridi ndio hao waganga wa kienyeji, na vikundi vya kishetani, pamoja na watu waovu wa ulimwengu huu. Lakini hao siyo wabaya sana. Wapo watumishi wengine wa uongo waliochaguliwa na shetani mahsusi kwa ajili ya kuwafanya watu wawe vuguvugu. Hawa ndio wale mbwa mwitu Bwana aliowasemea katikati ya kondoo, Mathayo 7:15 “Jihadharini na Manabii wa Uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa-mwitu wakali.
16 MTAWATAMBUA KWA MATUNDA YAO. Je! Watu huchuma zabibu katika miiba, au tini katika mibaruti? “
Unaona hapo. Hao wanabeba biblia kama wewe, wanajiita watumishi wa Mungu, na njia pekee ya kuwagundua si kwa kuwatazama, bali ni kwa matunda yao, kwa kutazama jamii ya watu wanaowazalisha (ndiyo matunda yao), utaweza kufahamu hao watumishi ni wa aina gani, kama ni vuguvugu, moto, au baridi.
Hata kama watafanya miujiza kiasi gani jiepushe nao. Bwana Yesu alisema. Mathayo 7: 22 “Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? 23 Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu”.
Injili hii unayoisikia kila siku, na hutaki kubadilika, unasema wewe ni mkristo, lakini ukiangalia maisha yako na maandiko ni mbalimbali, umejiweka katika eneo la hatari zaidi. Shetani anakufurahia kukuona katika hali hiyo, akisubiria hiyo siku Bwana atakayosema basi yatosha. Ili utapikwe, shetani anataka awe na uhakika wewe unakuwa wake milele. Hataki kukupoteza kwa namna yoyote ile na ndiyo maana anataka uendelee katika hali yako ya UVUGUVUGU. Ujione umempendeza Mungu kumbe unamchukiza, n.k, Ni mara ngapi umesikia sauti ya Mungu ikisema na wewe ndani ya moyo wako, lakini hutaki kubadilika.
Maneno ya Bwana Yesu ni kweli na Amina. Hasemi uongo wala hatanii akisema atakutapika, ni kweli atakutapika. Hivyo, mgeukie leo Bwana kikamilifu. Kama hujafanya hivyo toka katika kamba za kidini na madhehebu zinazokulewesha kukufanya ujione ni mkristo kumbe siyo, tafuta kweli ya Neno la Mungu kwa gharama yo yote ile.
Hili ndilo Shauri la Bwana Yesu kwako wewe wa Kanisa hili la Laodikia.
Ufunuo 3: 16 “Basi, KWA SABABU UNA UVUGUVUGU, WALA HU BARIDI WALA MOTO, NITAKUTAPIKA UTOKE KATIKA KINYWA CHANGU. 17 Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi. 18 Nakupa Shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona.
19 Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu.
20 Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami”.
Makanisa saba yaliyotajwa katika kitabu cha Ufunuo yalikuwa ni makanisa halisi. Ingawa yalikuwa makanisa halisi wakati huo, kuna maana ya kiroho kwa makanisa na waumini hii leo.
Dhumuni la kwanza ya barua walizoandikiwa makanisa hayo lilikuwa ni kukidhi mahitaji yao ya kiimnani wakati huo. Kusudi la pili ni kufunua aina saba za watu/makanisa katika historia na kuwafundisha ukweli wa Mungu. Kusudi la tatu ni kutumia makanisa saba kuashiria vipindi saba tofauti katika historia ya kanisa.
Kumbuka kuwa jumuiya za makanisa saba huko Uturuki ni mfano wa kanisa lote duniani kote. Tunaishi katika kipindi cha kanisa la saba na la mwisho la Laodikia, muda mfupi kabla ya unyakuo.
Kuna watu wako na imani vuguvugu katika kuitikia Neno la Mungu. Wako wengi. Yaani, hali ya kanisa la Laodikia imefikiwa. Shauri la Bwana Yesu ni kwamba, usiwe wa Kanisa la Laodikia. Usiwe Mkristo baridi, ambapo huna habari na Neno la Mungu. Wala usiwe Mkristo vuguvugu, ambapo mguu ndani, mguu nje, mara unasali, mara husali, uko kwenye starehe za kidunia.
Ukristo wako ni wako wewe binafsi. Huna ubia na Mkristo mwingine, kwani hukumu itatolewa kwako wewe kama wewe mtu binafsi. Hakuna hukumu itakayotolewa kwa makundi ya kifamilia au kirafiki wala ya kidhehebu.
Kusemwa ni jambo la kawaida. Usiogope wala kujali yatakayosemwa na waumini/wakristo wengine juu yako. Fanya uamuzi kuhusu maisha yako na hatima yako, yaani Ukristo wako na Kanisa lako. Hivyo, usiwe Mkristo baridi wala Mkristo vuguvugu. KUWA MKRISTO MOTO. Shika Neno la Mungu na kulitekeleza BILA WOGA NA BILA KUYUMBA.