Je, kati ya Machinga na Watumishi wa Umma, nani hasa wanaochafua miji?

Je, kati ya Machinga na Watumishi wa Umma, nani hasa wanaochafua miji?

Tazama Ramani

New Member
Joined
Dec 7, 2020
Posts
3
Reaction score
3
Salaam wanabodi,

Moja kwa moja kwenye hoja.

Tatizo tulilonalo ni ajira hii ni fact, watafiti wanasema kufikia 2050 Africa itahitaji ajira mpya zaidi ya milioni 500 (source frani hivi)

Hakuna serikali duniani iliomaliza tatzo la ajira kwa kuwaajiri wananchi wake wote (if I'm wrong, correct me) haiwezekani
Sekta binafsi ndio zinauwezo huo na hasa viwanda ndio mwarobaini.

Leo Bongo tunawatumishi wa umma wanaolipwa mishahara kwa Kodi za wananchi na hata posho kibao na hata magari ya umma, lakini hakuna kitu wanafanya zaidi ya kusaka rushwa kwa sekta binafsi, na kuzimaliza kwa ulevi na ngono, unawakuta wamenenepeana Kama vyura. Shame on them.

Leo tuna TANESCO yenye umeme wa koroboi kwa gharama kubwa, hauwezi kuendesha viwanda kwa faida.

Leo tuna TRA inayokusanya rushwa sio Kodi, yaani wanakukadiria Kodi kubwa ambayo huwezi kulipa, ili mzungumze Rushwa.

Leo wawekezaji wanatoa RUSHWA nyingi zaidi kuliko Kodi na tozo halali...na hata zile mashine za EFD hakuana mtu analipa hata kwa nusu ya hesabu, haiwezekani, mmemkamua rushwa.

Kwa makosoro mengi hayo yatoshe kuonyesha tatizo lilipo

Kila mwaka vijana wanamaliza Form 4 wengi wao wakiwa wamefaulu kwa kiwango cha F, F, F

Na wengine kwenda juu zaidi. Ajira hamna, unafikiri wanaenda wapi?

Unasema unawapanga wasiwe uchafu town sawa, ukimfungia huko kutwa nzima hajauza, ww unataka aende wapi sasa?

Hivi kweli tukikuchukua wewe tukakubana kweli kwelii, uwe machinga haswaaa, tukafunga account zako zote hamna pesa unapata, tukubane kabisa kiasawasawa uwe machinga fulani ivii. Halafu tukakutenge huko kwenye mipango miji, utatoboa wewe? Kama hujatoa machozi ya damu sjui.

Alafu sio kila mtu ni wa supermarket (This is Africa) kila mtu anawateja wake, wengine ni nguo za mitumba hizo za machinga, wewe supermarket sawa, ila umesahau hata ndugu zako wamejazana kijjn hawana hata uwezo was kula milo mitatu, ww mwenyewe umesomeshwa na mama yako anauza gongo na kilimo cha jembe la mkono, hukua hata unayajua mafuta ya mgando ya kujipaka, umefika mjn umevimba kifua mbele kama umepgwa ngumi ya mgongo, shame ona you.

Huwezi kushindana kusafisha mji wakati watu hawana ajira, skills, capital na idadi yao inakua exponentially, your missing the real problem. So you can't solve it

Hebu waacheni wapigane mikono wapangane wataelewana tu (I mean waasaidieni wafanye biashara wapate ugari)

Ninyi komaeni ku-nurture sekta binafsi kikweli kwelii kwa damu na maji sekta binafsi zikue (siunajua tena vita ya biashara)

1. Umeme wa uhakika, bei chee, umeme wa jero mtu kama n hm vurugu zote anafanya, viwanda vipige kazi usk na mchana bila shida,,, mambo yenu yale ya umeme wa mafuta mazito yashindwe na yalegee...

2. Kodi ndogo zinazolipika na wigo uwe kwa watu wengi zaidi kadri iwezekanavyo. Toa elimu ya kodi, kusanya kwa hekima bila kuua biashara (atakaezingua zaidi kamata, shitaki) hakuna mtu amefanikiwa duniani kwa kucheka na wakwepa kodi.

Ondoa tozo tozo zingine hazina maana ni ulaji wa watu flani tu, walipe kodi inayolipika, na kama mtu kweli biashara imeyumba mpeni neema nk nk

Na mambo ya kua na skilled labor wa kuendesha viwanda ni mhm sana,, sio hata a simple machine operator atoke china... Haiwezekani, Wabongo wanavipaji mnawaangaria tu mmekomaa na kuwakaririsha midude ambayo wanamaliza hamna kitu wanaweza kufanya, eti elim mara oooh wasomi wasomi hao kwiioo. Shabashii!

Malizieni reli na muitunze kwa gharama yoyote (kama mmashindwa mabasi ya mwendokasi sijui).

Yaani tz iwe mtu anawekeza anazalisha kwa lowest cost, anaishi kwa amani na usalama (ujambazi usio na mbele na nyuma, komesha), watu tuwe na amani na pesa zetu, na wale wengine eti magaidi, komesha (u know what I mean).

Na mambo yoote mnayoyajua ndio kikwazo kikubwa cha biashara deal nayo kisawa sawa.

Hakika watu watapata ajira na mitaji, watajiajili, wataaajili na wengine wengi tu, na badala ya kujipanga bararani watakua productive citizens.

Hakuna mtu anapenda kukaa barabarani, apigiwe kelele na honi na magari yenu ya misaada.
 
Nimejaribu kusoma kwa haraka haraka namna sisi watumishi wa umma tunavyo chafua mazingira, sikuona! Zaidi tu ya kutusimanga eti tumenenepeana kama vyura!

Yaani hata mimi mlinzi wa Halmashauri nimenenepeana kama chura! Aisee wewe MMACHINGA mbona umekasirika sana! Nani amekukorofisha kiasi hicho!!
 
Hahahaha wameniudhi Sana bro, Soma utaona shida ilipoanzia, wanajaribu kukata matawi sababu eti kukata mizizi ni kazi, kiukweli hawataweza kuondoa tatizo lenyewe hasa.

Sjui wanataka tuwe Kama vijana wa Ethiopia Kila siku wanakimbia nchi yao,,, mtu anafanya kazi ndani ya nchi yake ww badala ya kumsaidia, unaenda kumficha kwenye kichaka Cha usafi wa jiji.

Tuliowapa mamlaka ndio wametufikisha hapa, Sasa wasitusumbue kabla hatujawasumbua
 
Back
Top Bottom