Ngaliwe
Senior Member
- Dec 30, 2015
- 164
- 374
HOJA ya Katiba mpya imeanza tena kuibuka kwa kasi kidogo, kwa maelezo kwamba hiki ni kipaumbele cha taifa kwa sasa. Kwamba baadhi yetu wanaamini kwamba bila Katiba mpya hatuwezi kupiga hatua za maendeleo kama ambavyo tunatarajia.
Hakuna ubishi juu ya umuhimu wa Katiba kwa nchi yoyote, kwa kuwa Katiba ndiyo sheria mama na hiyo ndiyo mhimili wa sheria zingine zote, ni muhimu sana kwa taifa kuwa na katiba yake ambayo itaisaidia kufikia malengo ambayo watu wake wamejiwekea.
Pamoja na umuhimu huu, ni kweli kwamba Tanzania kama taifa kwa sasa tunahitaji kuwa na katiba mpya kama kipaumbele muhimu kuliko masuala mengine yanayolikabili taifa letu? Hili ni suala la mjadala lakini katika kujenga msingi wa hoja yangu ninaomba niongozwe na hekima hii ya Baba wa Taifa Mwalimu Kambarage Nyerere kuhusu umuhimu wa Katiba.
“Haijalishi mtakuwa na Katiba ya namna gani, kama nchi haina maadili ya Taifa yatakayomwezesha Rais kusema ingawa katiba inaniniruhusu kufanya hili, siwezi kulifanya kwa kuwa si Utanzania, au wananchi kusema hatuwezi kufanya hili kwa sababu siyo utanzania liwe limetoka kwa rais au rais kipeuo cha pili, vinginevyo wananchi watabaki kuwa waathirika wa udikteta.”
Mwalimu anasema nini, pamoja na umuhimu wa katiba lakini kwa yenyewe siyo kila kitu na kwamba kuwa na Katiba nzuri hakumaanishi ndiyo mwisho wa changamoto zote. Tukitaka kuwa wakweli tutatambua kwamba hatimaye bila maadili yanayowezesha utekelezaji makini wa katiba, haijalishi katiba hiyo inaandika na kutamka mambo mazuri kiasi gani, yanaweza kubaki kuwa maandishi tu bila kuwa na dhamira ya dhati ya utekelezaji.
Hii ndiyo kusema kwamba, kama tunayo dhamira na maadili mema yanayoliwezesha taifa letu kutekeleza mahitaji yake ya msingi kama vipaumbele vya kuwaletea watu maendeleo, hatuhitaji udharura wa kukimbilia katiba mpya kwa sasa, wakati maadili ya kitaifa hayohayo yanawezesha katiba iliyopo sasa kutekelezwa kwa manufaa makubwa ya taifa huku tukisukuma mbele vipaumbele vya kweli vya taifa na kuwaondolea wananchi umasikini.
Ni kweli kwamba wananchi walio wengi kipaumbele chao cha kwanza ni kupata barabara nzuri kwenye vijiji, mitaa na vitongoji vyao, wakulima wapate pembejeo kwa bei nafuu na uhakika wa masoko ya bidhaa za kilimo, vijana wapate ajira, mazingira mazuri ya uwekezaji na uanzishaji wa biashara, kuboresha huduma za afya, elimu na miundombinu mingine wezeshi kwa ajili ya kuweka mazingira mazuri ya kuendeleza taifa letu, haya hayategemei Katiba mpya.
Kama taifa lazima tujitafakari na kuona tunahitaji nini hasa kwa sasa, ni lazima ifike mahali tukubali kwamba pamoja na umuhimu wa harakati za masuala ya siasa katika nchi, lakini lazima yawe kwa kipimo na kiasi, nchi zote ambazo zimeendelea zilipiga hatua kubwa ya maendeleo walifika mahali wakitambua wanahitaji nini na kwa sababu gani bila kujali dunia ya nje inashinikiza nini.
Nchi nyingi hata za Ulaya zilifanya mapinduzi makubwa ya maendeleo kwa watu wao katika nyakati ambazo waliamua kuchagua kuelekeza nguvu zao kwenye mahitaji na vipaumbele vyao vya kweli bila kupelekwa pelekwa na mahitaji ya mataifa wengine, yenye maslahi zaidi na mashinikizo hayo kuliko tunaoshinikizwa.
Lipo kosa moja ambalo dunia inafanya, inashinikiza sisi nchi zinazoendelea turuke hatua ambayo mataifa makubwa walipitia wakiongozwa na mila na tamaduni zao lakini sisi wanataka turuke hatua hizo wakati wanajua fika kwamba kwa kufanya hivyo hawatusaidii kufikia kufikia malengo yetu, na kutufanya tuvurugikiwe na kuchanganyikiwa tu kama anavyokiri Mwanadiplomasia nguli wa Marekani, Dk. Henry Kissinger.
“West have fallen prey to the temptation of ignoring history and judging every new state by criteria of their own civilization. It is often overlooked that the institutions of the west did not spring full blown from the brow of contemporaries but evolved over centuries which shaped frontiers and defined legitimacy, constitutional provisions, and basic values.”
Kwa tafsiri isiyo rasmi anasema “Mataifa ya Magaharibi yameangukia katika mtengo wa kupuuza historia na kuyapima mataifa mapya kwa vigezo vya ustaarabu wao (wa Kimagharibi). Yanapuuza ukweli kwamba taasisi za kimagharibi hazikukua ghafla tu, isipokuwa zilijiimarisha tarataibu kwa karne kadhaa ili kujenga uhalali, katiba na msingi ya maadili.”
Sisi pia tunataka kuingia katika mtego huu, tunataka kujipima kwa viwango vya mataifa ambayo, Marekani kwa mfano, ina umri wa miaka 245 ya uhuru. Tangu ilipopata uhuru toka kwa Waingereza Julai 04, 1776 Taifa hilo limepita katika hatua nyingi mno za hovyo na za maana, mpaka kufika hapa lilipofika, lakini likiongozwa na mila, utamaduni na historia yake.
Tanzania katika umri wake wa miaka 60 ya Uhuru, haimaanishi tupite kila aina ya madhira waliyopitia, hilo haliwezekani kutokana na tofauti za mazingira, utamaduni na nyakati. Lakini ni muhimu sana kutambua kwamba pia hatuwezi kupiga hatua za maana kwa kuiga kila kitu chao kwa sababu zile zile za historia, utamaduni na nyakati, tunachotakiwa kufanya ni kujiruhusu sisi kama taifa kukua na kujiimarisha katika misingi ya maadili na mfumo wa utawala unaozingatia misingi ya historia yetu, mila na utamaduni wetu.
Na kwa hili la katiba, tunafanya haraka isiyokuwa na sababu, kwanza kwa sababu siyo kweli kwamba hiki ni kipaumbele cha taifa, lakini pia kama alivyosema Baba wa Taifa hapo juu, maadili ya utaifa wetu kwa sasa yanatosha kabisa kuendelea kulijenga taifa letu kwa katiba iliyopo.
Wapo watu wanalinganisha na nchi jirani, Kenya kwa Katiba yao mpya, lakini liko jambo hawalioni wala hawataki kulijadili jinsi katiba hiyo inavyowaingiza kwenye migogoro kila uchao hali inayoliweka pia kwenye hatari ya kutumbukia kwenye migogoro isiyokoma (tutalijadili kwa upana hili wakati mwingine).
Itoshe tu kuhitimisha hapa kwamba, tukiamua kuwa wakweli kwa dhati za utambuzi wetu na kwa kuzingatia hali halisi nchini, utaona kwamba vipaumbele halisi vya taifa letu kwa sasa ni huduma za maji, umeme wa uhakika, huduma za afya na dawa, miundombinu, viwanda na miradi ya kimkakati inayoweza kuiweka Tanzania katika ramani ya ushindani katika uwekezaji kwenye ukanda huu wa Afrika na siyo katiba mpya.
ASANTE SAMIA