Je, Katiba mpya ni mhimu kwa sasa?

Je, Katiba mpya ni mhimu kwa sasa?

ONJO

JF-Expert Member
Joined
Jun 1, 2022
Posts
216
Reaction score
265
Habari zenu wanaharakati..

Nimekubali kuwa mjinga ili nielewe umhimu wa kuwa na katiba mpya.

Najieleza, katiba ni muhimu kwa nchi yeyote kwani ndiyo inayotoa mwongozo katika utungaji wa sheria na kanuni, na ni mwongozo katika utekelezaji wa miradi ya kimaendeleo hasa taifa la tanzania.

Hoja yangu ya msingi ni kwamba pamoja na dosari ambazo zipo kwenye katiba yetu. Je, zikirekebishwa zitaweza kusukuma maendeleo kwa kasi? Au tutahitaji tena kuwa na kiongozi mwenye maono?

Je ndio kusema Tanzania ni masikini kwakuwa katiba yake ni mbovu?

Tuwekane wazi wanaharakati ili tujue kuamua kipi ni kizuri na kipi ni kibaya.

Na ONJO mpenzi wenu.
 
Kama huoni tatizo la katiba iliyopo,wewe ni mtu wa ajabu sana na hapa jamiiforum uhame haraka
 
Umasikini wa akili ni hatari kwa taifa letu katiba yetu inaruhusu uhuru wa kutoa maoni ni afadhali wewe uhame kabisa.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]ni kweli huoni tatizo la katiba hii??au unatania??
 
Katiba ndiyo sheria mama?
Kama ni ndiyo unahisi sheria zetu ni kali kwa kiasi gani? Mf ile ya pccb 2007?
Raisi ni binadam? Nn kitatokea kwa madaraka makubwa ya kikatiba aliyonayo hasa akitokea raisi fyatu kama jpm?
Kura za uraisi wanapiga wtz? Kwann zisihojiwe. Mahakamani?
Wazir ni mbunge ndiyo ukitaka kumuajibisha unafanyaje?
 
Habari zenu wanaharakati..

Nimekubali kuwa mjinga ili nielewe umhimu wa kuwa na katiba mpya.

Najieleza, katiba ni muhimu kwa nchi yeyote kwani ndiyo inayotoa mwongozo katika utungaji wa sheria na kanuni, na ni mwongozo katika utekelezaji wa miradi ya kimaendeleo hasa taifa la tanzania.

Hoja yangu ya msingi ni kwamba pamoja na dosari ambazo zipo kwenye katiba yetu. Je, zikirekebishwa zitaweza kusukuma maendeleo kwa kasi? Au tutahitaji tena kuwa na kiongozi mwenye maono?

Je ndio kusema Tanzania ni masikini kwakuwa katiba yake ni mbovu?

Tuwekane wazi wanaharakati ili tujue kuamua kipi ni kizuri na kipi ni kibaya.

Na ONJO mpenzi wenu.
Mkuu; Unayo hoja nzuri lakini pia zingatia kwamba katika hali ya maisha ya kawaida hebu fikiria Katiba iliyopo kwa sasa ni ya 1977 ina umri wa miaka 46+ ingekuwa ni mtu basi huyo ni mtu mzima sana(Mzee). Kama ni imezeeka maana yake ilishafanyiwa marekebisho mengi sana kiasi kwamba kama ingekuwa ni nguo ya kuvaa tunasema imejaa viraka vingi mno.
Kumbuka Katiba kama ulivyosema ndo Mwongozo wa Nchi. Kwa maneno mengine Katiba ndo inasimamia na kuamua Mustakabali wa maisha na Maendeleo ya Watanzania kwa ujumla ya kila siku. Wanaofanya marekebisho ya Katiba hujikita tu kwenye baadhi ya sehemu ambazo ni zile zenye hitajio la marekebisho. Kwa mantiki hiyo inawezekana kukawa na sehemu inayohitaji marekebisho lakini haikuzingatiwa. Hilo ni mapungufu.
Katika Utekelezaji na Usimamizi, Rais ndio mwenye jukumu hilo. Kama Katiba ina mapungufu na yeye kama Rais aliapa kuilinda Katiba hiyo ina maana atalinda hata hayo mapungufu. i.e Katiba inaweza kuwa ni kikwazo katika utendaji wa shughuli za siku hadi siku za Rais na Viongozi wenzake Akithubutu kufanya tofauti eti ni kwa nia njema, atatokea kidudu-mtu na atakuwa na haki ya kupeleka malalamiko mahakamani ili haki itendeke.
Vinginevyo itaweza kuleta mtafaruku ndani ya Taifa. Kwa mantiki hiyo ili tuweze kuenda kwa pamoja na kuondoa dhana ya uzee wa Katiba iliyopo na mapungufu yake, ni bora na inafaa kuwepo kwa Katiba mpya itakayo kuwa tumeiandaa sote kwa pamoja na kuikubali sote kuliko hii iliyopo ambayo wengine hatuitaki na huku wengie wanaridhika nayo huku wengine wamekaa kimya kusubiri kitakachoendelea. Pia maadui wa nchi (wa ndani na nje) watapata mwanya wa kujipenyeza kwetu kwa hoja ya Katiba chakavu. Kwa maneno mengine tukubali kuingia gharama kwa kuendesha mchakato wa Katiba mpya ili tuweze kukwepa Gharama kubwa kuilinda Katiba chakavu iliyopo. Hiyo Katiba mpya haitajalisha hata kama 80% ya contents ni hizo-hizo zilizopo kwenye ya 1977 bali itakuwa ndiyo Katiba Tuliyo iandaa na kuikubali sote kwa pamoja. Katiba mpya.
 
Sawa kiongozi
 
Katiba ndiyo sheria mama?
Kama ni ndiyo unahisi sheria zetu ni kali kwa kiasi gani? Mf ile ya pccb 2007?
Raisi ni binadam? Nn kitatokea kwa madaraka makubwa ya kikatiba aliyonayo hasa akitokea raisi fyatu kama jpm?
Kura za uraisi wanapiga wtz? Kwann zisihojiwe. Mahakamani?
Wazir ni mbunge ndiyo ukitaka kumuajibisha unafanyaje?
Sawa kiasi kwamba ukimtumbua waziri anarudia ubunge.Hoja ni kwamba ukimfukuza arudi kwao nimekupata.
 
Mkuu umeeleza vizuri Sana ila tunahitaji kuwa nakatiba kwasabu katiba tulionayo niya 1977, hivyo mambo nawakati vinabadilika , kutokana namabadiliko hayo tunahitaji kuwa na katiba mpyaa
 
Back
Top Bottom