mwanalumango
JF-Expert Member
- Dec 13, 2010
- 232
- 279
Nachokoza tu kwa weledi wangu mdogo kuwa kutafuta rafiki wa kimahaba kwa minajiri ya kuwa mchumba na hatimaye my wife/husband ni kigezo kisichokuwa na msingi na ni cha kibaguzi na unyanyapaa wa wasiosoma. Si lazima iwe sahihi sana ila kuna sababu zinazojitokeza kwenye maisha halisi ya Kitanzania inayoonesha kuwa Elimu si kipimo kizuri sana cha mtu kuwa mume/mke bora na kuwa na ndoa iliyotengemaa.
Angalia matokeo ya tafiti za kienyeji katika maisha ya kawaida ya Kitanzania:
- Mahusiano mengi ya Aliyesoma hususani mwanaume na asiyesoma mwanamke yamekuwa ya kudumu sana. Itilafu inatokea pale mmoja anapoona kuwa yeye ni bora zaidi ya mwenza wake kwa ajili ya elimu aliyonayo, lakini kama hilo halipo mahusiano huwa ni ya kudumu zaidi
-Unapolala na mwenza hulali na degree wala udaktari bali unalala na mpenzi, raha na starehe zinazopatikanika hazinamahusiano kabisa na elimu ya mtu.
- Heshima katika mahusiano haitokani na elimu bali malezi bora toka kwa wazazi. Mwenza anaweza asiwe na elimu bali akashehena mambo muhimu katika mahusiano pamoja na mapenzi ya kweli, uadilifu, uchapakazi, hutuma, upenda kwa mwenzake na familia yake kwa jumla na kupelekea kuwa muhimili wa mahusiano
- Sioni sababu kwanini wasio na elimu fulani wa baguliwe, kwa mimi hakuna sababu ya kufanya hivyo kwakuwa kuna wengi wasionaelimu wamefanikiwa sana kimaisha na kiuchumi, wamekuwa wafanyabiashara wakubwa, wamekuwa na vipaji vikubwa.
- Mahusiano mengi ya wasomi yana migogoro sana, jipime wewe au unaowafahamu
Kwahiyo elimu bado sio kigezo katika kutafuta mahusiano bora na ya kudumu, wengine watasema exposure, lakini wewe uliyesoma unaweza kumfanya uliyenaye awe vyovyote unavyotaka wewe kama kweli unampenda. tusiogope sana ugumu wa maisha kwakutafuta mpenzi msomi unayetaka msaidiane naye na ukapoteza raha ya mapenzi katika maisha yako yote.
NAOMBA NIFAHAMISHENI KWANINI TWATUMIA KIGEZO CHA ELIMU? Nataka mtu anieleze objectively nini hasa. Mwisho natoa siri, mimi ni msomi wa kiwango cha juu kabisa na niko well exposed, nimefanyakazi nchi mbalimbali katika mabara yote karibuni na watu wa mataifa mbalimbali, na mke wangu hakusoma kabisa lakini we have been in a wonderful relationship, she is everything to me, sijaona kushindwa kufanyakitu kwakuwa hana elimu kubwa na sijaona kushindwa kutimiza majukumu yake kama mama wa familia na mzalishaji kiuchumi anapowezeshwa eti kwakuwa hana elimu. Naomba nielezeni nini kigezo hasa cha kubagua wenza kutokana na elimu.