Je, kilichotokea Malawi kinajirudia Zambia ambapo Rais anatimuliwa?

Father of All

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2012
Posts
7,672
Reaction score
9,039
Hamjambo wana jamvi? Hali ni tete kwa Rais wa Zambia Edgar Lungu. Lungu la wapiga kura limemshukia huku mpinzani wake mkuu Hakainde Hichilema akizidi kuchanja mbuga kumnyang'anya Ikulu.

Sisi kama majirani na marafiki tunaangalia kwa jicho la karibu. Je kilichotokea Malawi ambapo upinzani uliingusha serikali iliyoko madarakani kinajirudia Zambia? Je watanzania tunajifunza nini?

Inakuwaje viinchi vidogo vinatushinda?
 
We Mzee huu nao utauita Uzi?????
Nyama amna
 
Hizo ndio nchi bwana. Mwaka huu chama hiki, mwaka mwingine chama kingine. Lazima anaeingia madarakani achape kazi, kwasababu ya kuhofia wananchi kumshukia kwa kura.

Nasikitika sana sisi Watanzania kura zetu hazina maana yoyote. Nimeapa haitotokea kupiga kura tena
 
Hata police wetu awaamini bila ccm maisha yanaweza endelea.
Nchi sio mtu sio chama. Kaondoka Nyerere, Magu tunasonga tu.
 
Huku tuna maisha yetu tushazoea hatuna muda najua mnapenda zitokeee lakini kwa uwezo wa Allah hakutotokea chafuko lolote
 
Yaan tuiondee CCM wakati wapinzani wenyewe hawana demokrasia? Yaan Mbowe mwenyekiti wa kudumu halafu unafikiria kuiondoa CCM. Mzee jaribu kuja na hoja za maana.
 
Sio kwamba vi nchi vidogo vinatushinda. Ila ukweli ni kuwa katiba zao zina unafuu kuliko hii ya kwetu. NdIo maana inakuwa rahisi kwa wapinzani kupindua meza wakikaza. Bongo lazima tupiganie katiba mpya na tume huru kama tunataka tutoe chance kwa wapinzani kuingia madarakani. Lasivyo kwa katiba hii, njia inayobaki ni ya mapinduzi ndo wengine wataweza kuingia madarakani.
 
Yaan ,tuiondea ccm wakati ,wapinzani wenyewe hawana demokrasia?Yaan Mbowe mwenyekiti wa kudumu.Halafu unafikiria kuiondoa ccm.Mzee jaribu kuja na hoja za maana.
Acha hizo fikra unajua HH amekuwa kiongoz kwa muda gani kwenye chama chake, ukwel mchungu vyama vya upinzan vinahitaji viongoz dhabiti kwa ajili ya kupambna na chama tawala.. angalia historia ya vyama vingi vya upinzan Afrika ambayo baadaye vilishika uongoz, viongoz wao walikaa madarakn muda mrefu kabla ya kufanikiwa kuingia ikulu
 
Zambia ndiyo nchi iliyobadilisha marais kwa sanduku la kura mara nyingi zaidi Barani Afrika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…