Je, Kinana ni mzalendo?

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
7,823
Reaction score
10,857
Nikiwa mdogo mwaka 1986 jirani yetu ambaye alikuwa anakaa kwenye nyumba za msajili njia ya Sanawari. Alikuwa mpole, mrefu na anaonekana tofauti sana kulinganisha na vijana wengine pale.

Mzee wangu ambaye alikuwa mmoja wa viongozi wakuu wa mkoa wa Arusha alialikwa kwenye harusi ya Kinana! Cha ajabu huyu kijana alikuwa kapata Ubunge na kuchaguliwa Naibu Waziri wa Ulinzi.

Mtaa mzima tulikula pilau karibu wiki nzima na Waziri wa Ulinzi wa wakati huo Salim Salim alikuja kwenye harusi ile ya mkeka na waligawa video tapes za harusi kila mahali. Kiukweli Kinana alikuwa anapedwa kama mfalme wa Arusha mjini miaka hiyo.

Baadae tukaanza kuona dry cleaners za wasomali na kuambiwa za Kinana!. Baadae Kinana akawa anajiona tofauti sana na wakazi wa kawaida nakumbuka vijiwe vya chai alikuwa hawezi kwenda tena.

Na ghafla Kinana akaanza kuwa mwongeaji zaidi🤔 sio yule mpole. Lakini Arusha ikaanza kubadilika kutoka kuwa mji wa Wamasai kuanza kuwa mji wa Wachagga. Miaka ya 90’s Arusha Mjini ukawa mji wa wafanyabiashara wahamiaji kutoka mji wa Moshi.

Wafanyabiashara wengi wa Kimasai ambao walikuwa wana support sana CCM na Kinana walihamia kwenye mashamba yao Arumeru, migodini na biashara nyingine baada ya wachagga kuleta ushindani mkubwa sana Arusha. Lakini wale wahindi wengi wa Arusha wenye pesa walibaki bila chama maana upepo ulikuwa unaenda upinzani.

Arusha walikuwa hawapendi serikali kwasababu ilikuwa haina mradi wowote pale mjini wa maana. Majengo yalikuwa na wauza mawe na wahindi na sio kampuni za Serikali au za pesa kama Dar.

Kinana naye akaja kama mfanyabiashara! Akafungua kampuni zake za utalii na uwindaji. Sawa kila majambazi wa kisomali wakishikwa kuna note inatoka juu zaidi Serikalini inasema waachiwe ni ndugu wa Kinana! Hii ni mpaka leo hii🤔. Gafla miaka ya 90’s Kinana akawa mfanyabiashara kuliko mwanasiasa na alipoteza watu wote waliokuwa wana msupport pale mjini.

Wakati huo kulikuwa na kikundi cha Wambulu wakiongozwa na tajiri wa magari Verani ambaye ndiye alikuwa mbebaji wa ngano za kampuni ya bia Tanzania nzima kutoka pale Karatu.

Wambulu wakakutana miaka hiyo na kumchagua kinara wao ambaye ndiye Sumaye awe mbunge ili nao wapate nguvu Arusha. Lakini baada ya kuona maji mazito sumaye alienda kugombea kwao na kubahatika kuwa Waziri! . Alivyokuja Mkapa na kumpa Sumaye Waziri Mkuu Sumaye akaja Arusha na kusema yeye ndiye king mpya wa Arusha na sio Kinana. Kitu cha kwanza sumaye alifanya kushindana ni kuwapa vitalu wambulu mbuguni baada ya miaka michache akatokea king of Tanzanite ambaye alikuwa na jina na Sunda! ambaye alikuwa kijana wa Sumaye.

Hili la Sumaye likamkimbiza kabisa Kinana na mpaka leo Kinana sio yule mzalendo ambaye alikuwa mbunge 1986.

Nasema haya na kumwonya Rais awe makini na Kinana ni mfanyabiashara hana mapenzi na mtu. Yeye anaona kama vile ana kazi na sio wito

Je, alisingiziwa hapa🤔?

The country's Natural Resources and Tourism Minister Khamis Kagasheki admitted to amaBhungane that politicians are involved in the ivory trade.

“This business involves rich people and politicians who have formed a very sophisticated network,” Kagasheki said.

His deputy, Lazaro Nyalandu, echoed this, saying that big names in the Cabinet and the army, as well as officials in wildlife conservation, the Tanzanian Port Authority, the immigration department and the police, are implicated.



“It is a hard fight because the network collaborates as a team, sharing information, money and positions,” Nyalandu said.

Shein
A report read by the main opposition party, Chadema, in Parliament in June pointed a finger at a member of the ruling Chama Cha Mapinduzi (CCM) party, wealthy businessperson Mohsin Abdallah Shein.

Shein was said to own 16 hunting blocks in game reserves. He allegedly uses these for poaching.

The hunting blocks are held by four companies – Royal Frontiers of Tanzania Limited, Game Frontiers of Tanzania Limited, Western Frontiers of Tanzania Limited and Northern Hunting and Enterprises Limited – which local media alleged belong either to him or his relatives.

This week, Shein described himself as “an innocent citizen of Tanzania” who is being targeted by business competitors.

“I've never been involved in illegal business, let alone elephant tusks,” he told the Mail & Guardian.

“I have a number of legal businesses and I don't see the point of it.”

Shein said that he owned Game Frontiers of Tanzania, but that the company operates “according to the law. These heavy allegations are full of lies.” He vehemently denied owning 16 hunting blocks.

Kinana
Another powerful figure under suspicion is the CCM secretary general, Abdulrahman Kinana.

In 2009, customs officers at the Vietnamese port of Haiphong found tusks weighing a massive 6.2 tonnes under bags of plastic waste on the freighter Sharaf.

The Sharaf Shipping Company, which owns the Sharaf, was registered in October 2003 in the name of Kinana and his wife.

Kinana insists he did not know about the hidden cargo. This week he said that both Interpol and the Convention on International Trade in Endangered Species had cleared him of any wrongdoing and that he was a victim of a politically motivated smear campaign.

Yaani eti huyu ndiye alikuwa awe next Salim salim. Hakunaga copy ya kipaji!

 
Akili za kimasikin zinakera sana so ukiwa mfanyabiashara ndio sio muadilifu sio?
Kuna vimaneno kwenye bandiko lake ama umeviruka Bahati mbaya ama umeviruka Bahati makusudi. Vinginevyo, usingeibuka na swali hili. Hata hivyo, Mimi naamini katika ushahidi usiotiliwa mashaka. Naamini, Makamu Mwenyekiti ni msafi mpaka hapo itakapodhibitika vinginevyo.
 
Kinana huwa anaombwa kusaidia...hajawahi kutaka mwenyewe kuongoza....Hana maneno mengi...anajua mipango..he is a winner....born winner ...the rest majungu
Uraia wa Kinana ni HIGHLY HIGHLY questionable. Yeye na kina Kikwete, Makamba na Lowassa wanafahamu fika.
 
Mkuu @kamindu, Kinana ni mmoja wa wazalendo wa kweli wa nchi hii!. Ni Kinana na Nape ndio wameiokoa CCM ile 2010 to 2015 kwa zile ziara zao za amsha amsha, baada ya kusoma bandiko hili CCM Imechokwa, CHADEMA Haijajipanga!, kwenye bandiko hili nilishauri
Ushauri huo ulifuatwa immediately, CCM wakamtoa Makamba, wakamuingiza Kinana, Nape na January na hapa ndio survival ya CCM ilipoanzia maana ilikuwa almost dead! Chadema ilikuwa wachukue nchi Yametimia!, CCM Imechokwa!, CHADEMA Njia Nyeupe 2015!-Jipangeni! hapa ni Kinana ameiokoa CCM!.

Baada ya issue ya uraia wa Azim Premji kuibuka, Kinana alirekebisha uraia wake kwa official declaration kama Bashe na Jenerali Ulimwengu, ila kiukweli kabisa kuna watu kibao tuu ambao sio raia wa Tanzania lakini ni wazalendo kuliko Watanzania wenyewe!, watu kama Joan Wickens, Amiri Jamal, Dr. Leader Starring, Oscar Kambona, Michael Kamaliza, Chinyama Chiume etc, hivyo Kinana ni mzalendo wa kweli kabisa wa Taifa hili!.

Kitendo cha Kinana kutukanwa na yule kichaa ile 2015 na ule ukichaa wa voice notes ulimfedhehesha sana Kinana nami niliuzungumza hapa, Psychoanalysis ya Waomba Msamaha Kwa Rais, Makamba Snr is the Next, Membe Will Never for Pride, Kiburi na Jeuri, Kinana Will Never for Integrity humu nilisema
Natumaini wale mnao ijua karma by now you can connect the dots usikute karma ya Kinana imechangia kwenye ile issue na huku kuwa elevated ni karmic consolations kumfidia!.
Nasisitiza Kinana ni mzalendo, and also karma is real, mtu akiwa mzalendo wa type kama ya Comred Kinana, mtu uki doubts uzalendo wake, ukaandika au kumshitumu, watu wakianza kum doubts kutokana na andiko lako, chochote negative kitakacho sababishwa na andiko lako, kitakuwa na karmic consequences
P.
 
Sunda ni mbulu?Kweli wajinga wengi.Hii hadithi isiyokuwa na kichwa wala miguu.Kinana kazaliwa Mbuguni kuna mjinga anadai eti "uraia" wake una utata!
 
kijana alikuwa kapata ubunge na kuchaguliwa waziri mdogo wa ulinzi.
Unamaanisha naibu waziri ?

Nasema haya na kumwonya Raisi awe makini na kinana ni mfanyabiashara hana mapenzi na mtu. Yeye anaona kama vile ana kazi na sio wito
Viongozi wote wa Sasa ni wafanyabiashara hata Ccm ni chama cha wafanyabiashara na matajiri wenye ukwasi....acha kumlenga Kinana pekee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…