Je, kipimo cha full blood pictures kinajumuisha vipimo vyote pamoja na Ukimwi?

Je, kipimo cha full blood pictures kinajumuisha vipimo vyote pamoja na Ukimwi?

The Boss

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2009
Posts
49,282
Reaction score
117,244
Wataalam

Ningependa kujua kwa undani maana ya hiki kipimo cha full blood picture

Kinahusu vipimo vyote vya damu? including HIV?
Au ni vipi?

Je, kinamsaidia dokta kupata picha ya magonjwa mengine kabla ya kupima?
 
I too want to know.... alafu last time nilifanya hio kitu but hata wazo la kujiuliza

Ulicho jiuliza halikuwepo kabisa.... Thus very interesting....

unajua hata mimi nashangazwa na jinsi Madaktari wanavyokipa umuhimu hiki kipimo
na kila nikipima na kuonyesha hakuna tatizo.

Ni kama wana dismiss haja ya kupima vipimo vingine...

Sasa ndo najiuliza, hiki kipimo ni nini hasa?
 
unajua hata mimi nashangazwa na jinsi Madaktari wanavyokipa umuhimu hiki kipimo.

Na kila nikipima na kuonyesha hakuna tatizo ni kama wana dismiss haja ya kupima vipimo vingine...

sasa ndo najiuliza,hiki kipimo ni nini hasa?

Hapo ndio tusubiri wataalam wamalize Rounds za clinic na kupunguza wagonjwa then watinge JF....
 
kaka we nenda moja kwa moja ukacheki digambo - mambo ya kuanza ku beep kwa full blood picture ya kizamani hayo. dawa si zipo unaogopa nini?
 
kaka we nenda moja kwa moja ukacheki digambo - mambo ya kuanza ku beep kwa full blood picture ya kizamani hayo. dawa si zipo unaogopa nini?

dawa za kutibu nini zipo?
 
Full Blood Picture (FBP)...au kwa kitaalam zaidi inaitwa Full Blood Count (FBC) au Complete Blood Count (CBC) ni kipimo cha damu ambacho majibu yake yanaonyesha mgawanyiko au kiasi cha seli (cells) mbali mbali kwenye damu.

The Idea is, mtu unapokuwa mgonjwa...mwili wako unarespond au kureact kwa kile kinachosababisha ugonjwa huo, mara nyingi kwa kutumia seli (cell mediated immunity) au chachu kama antibodies (Humoral immunity) kushambulia hicho chanzo cha ugonjwa mfano bacteria, virus etc.

Sasa FBP/FBC/CBC inaangalia mabadiliko ya seli katika damu ili kuweza kupata idea (sio kuconfirm) kama kuna infection, na kama ipo basi labda ni ya asili gani (mara nyingi seli zinazorespond kwa bacterial infection ni tofauti na za viral infection)...zaidi ya kutoa mgawanyo wa seli, test hiyo pia hutoa kiasi na size (in volume) ya seli nyekundu hivyo kutoa idea kwa wagonjwa wenye upungufu wa damu basi unaweza kuwa upungufu wa aina gani (microcytic/megaloblastic anaemia) ambao unaweza kusaidia kutambua aina tofauti za upungufu wa damu.

Kwenye ile fomu ya majibu, mgawanyiko/kiasi cha seli kwenye damu ya mgonjwa hulinganishwa na viwango standard (normal range) ambapo ukilinganisha unaweza jua kuwa viwango vimeongezeka au kupungua kutoka kwenye normal range. Pia kwa wataalamu waliobobea kwenye mambo ya damu wanaweza soma zile graphical presentation ili kuona mengi tu.

LAKINI: FBP/FBC/CBC haitoi majibu ya HIV. Test ya HIV inapima antibodies (Humoral), japo kuna madaktari kwa kuangalia mgawanyiko wa seli anaweza akahisi unaweza kuwa na chronic illness (kuna cells hasa Lymphocytes) huwa zinabadilika mganyiko wake kwenye damu kama mgonjwa ana ugonjwa sugu including HIV and TB. Hivyo Dr anaweza kutumia majibu ya FBP kukushauri ukafanye kipimo cha HIV ili kuthibitisha.
 
Full blood picture ni kipimo kinachoonyesha hali ya damu, yaani kama kwenye damu kuna mapungufu/matatizo. Kunapimwa: haemoglobin (HB) level (yaani uwingi wa damu), uwingi wa red blood cells, uwingi wa white blood cells kwa jumla na aina mbalimbali.

Kipimo cha HIV hakimo. Ni kipimo cha jumla sana kwa sababu hakilengi ugonjwa wowote. Kama majibu yake hayatakuwa normal, itamaanisha kuwa mgonjwa ana tatizo la kiafya, lkn haitajulikana moja kwa moja ni tatizo gani. Vipimo vingine itabidi vifanywe ili kujua aina ya tatizo/ugonjwa.

Nadhani nimeeleweka, japo kidogo. Ni vigumu sana kufafanua mambo ya medicine kwa lugha ambayo kila mtu ataelewa
 
Je ni dawa gani unaweza kutumia kuweka kwenye choo chako ili kuzuia infection kwenye choo chako?

Niliwahi kuona ikiwa imewekwa kwenye choo ni ya rangi ya bluu nikiwa kwenye nyumba flani nilikokuwa nimetembelea ila sijui kama ndiyo yenyewe
 
the boss naona majibu uliyopata yametosheleza. fbp haipimi hiv,nia ni kuangalia hali ya damu na kama kuna chronic infection inamsaidia dr wako kukupa ushauri zaidi
 
chooni unatakiwa kutumia disinfecttant yoyote ile. wakati wa kusafisha ndo muhimu zaidi. japokuwa zipo zile za kutundika kwenye flashing tank au kwente choo (cha kukaa) nazo ni nzuri. jik ni mojawapo ya disinfectant nzuri sana na inang'arisha pia (ina chlorine,inaua vijidudu vyote sugu) japokuwa harufu yake sio nzuri sana. mara nyingi rangi inatumika ya blue ama kijani, japo kuna za pink pia. huo ni utashi tu wa mtengenezaji,zisikubabaishe.
Je ni dawa gani unaweza kutumia kuweka kwenye choo chako ili kuzuia infection kwenye choo chako?Niliwahi kuona ikiwa imewekwa kwenye choo ni ya rangi ya bluu nikiwa kwenye nyumba flani nilikokuwa nimetembelea ila sijui kama ndiyo yenyewe
 
dawa za kutibu nini zipo?

dawa ya ukimwi si ipo hakuna haja ya kubeep kwa kupima full blood picture - ile inampa daktari dalili tu lakini lazima uende vipimo vya ndani. wengi hupima hiyo kabla ili kujiondolea wasiwasi.
 
Je ni dawa gani unaweza kutumia kuweka kwenye choo chako ili kuzuia infection kwenye choo chako?
Niliwahi kuona ikiwa imewekwa kwenye choo ni ya rangi ya bluu nikiwa kwenye nyumba flani nilikokuwa nimetembelea ila sijui kama ndiyo yenyewe
halafu wewe umenifurahisha naona kama umedandia lile daladala la bi kiroboto:biggrin1: you know what i mean " mada" ila hiyo dawa nafikiri ziko za aina tofauti tofauti i.e. Harpic.
 
Tunashukru kwa elimu yenu maana afya ni muhimu sana kwa hiyo inasaidia sana endapo unapata elimu hata kama hauumwi lakini ni vizuri kujua afya
 
Back
Top Bottom