Full Blood Picture (FBP)...au kwa kitaalam zaidi inaitwa Full Blood Count (FBC) au Complete Blood Count (CBC) ni kipimo cha damu ambacho majibu yake yanaonyesha mgawanyiko au kiasi cha seli (cells) mbali mbali kwenye damu.
The Idea is, mtu unapokuwa mgonjwa...mwili wako unarespond au kureact kwa kile kinachosababisha ugonjwa huo, mara nyingi kwa kutumia seli (cell mediated immunity) au chachu kama antibodies (Humoral immunity) kushambulia hicho chanzo cha ugonjwa mfano bacteria, virus etc.
Sasa FBP/FBC/CBC inaangalia mabadiliko ya seli katika damu ili kuweza kupata idea (sio kuconfirm) kama kuna infection, na kama ipo basi labda ni ya asili gani (mara nyingi seli zinazorespond kwa bacterial infection ni tofauti na za viral infection)...zaidi ya kutoa mgawanyo wa seli, test hiyo pia hutoa kiasi na size (in volume) ya seli nyekundu hivyo kutoa idea kwa wagonjwa wenye upungufu wa damu basi unaweza kuwa upungufu wa aina gani (microcytic/megaloblastic anaemia) ambao unaweza kusaidia kutambua aina tofauti za upungufu wa damu.
Kwenye ile fomu ya majibu, mgawanyiko/kiasi cha seli kwenye damu ya mgonjwa hulinganishwa na viwango standard (normal range) ambapo ukilinganisha unaweza jua kuwa viwango vimeongezeka au kupungua kutoka kwenye normal range. Pia kwa wataalamu waliobobea kwenye mambo ya damu wanaweza soma zile graphical presentation ili kuona mengi tu.
LAKINI: FBP/FBC/CBC haitoi majibu ya HIV. Test ya HIV inapima antibodies (Humoral), japo kuna madaktari kwa kuangalia mgawanyiko wa seli anaweza akahisi unaweza kuwa na chronic illness (kuna cells hasa Lymphocytes) huwa zinabadilika mganyiko wake kwenye damu kama mgonjwa ana ugonjwa sugu including HIV and TB. Hivyo Dr anaweza kutumia majibu ya FBP kukushauri ukafanye kipimo cha HIV ili kuthibitisha.