Hakuna lugha ambayo haijakopa kutoka lugha nyingine, kwani lugha ni sawa na mahusiano ya watu au mataifa mbalimbali, kuchanganyika kwao ndio kunakopelekea baadhi ya maneno ambayo lugha moja kuazima kutoka lugha nyingine, hali hii uitwa kutohoa, na wakati mwingine neno kamili linashindikana kutoholewa na kubaki kama lilivyo au kutafuta msamiati mpya kwa ajili ya ilo neno kutoka lugha moja kwenda lugha nyingine.
Leo hii tunabishania maneno ya kiingereza kwenda kwenye kiswahili, na hali tunasahau kuwa kuna maneno ya kiswahili ambayo hayapo kwenye Kiingereza.
Waswahili wana maneno ambayo pia tumeyatoa kwenye lugha nyingine na kuyafanya kuwa yetu kama vile, Pilau, Biliani, chapati, (Kihindi), na kuyaweka kwenye msamiati wetu, vilevile kuna maneno kama Wali, Mchele, Ubwabwa, K/Vitumbua maneno ambayo kwa Kiingereza hayapo. Zaidi ya neno mchele (Rice) hawana tena neno lingine kutofautisha kati ya wali, ubwabwa, pilau na biriani. Kuna neno kama Ugali, mlenda, mchicha n.k
Vile vile tuna maneno kama Bwana shamba, lala unono, mwiko, upawa (vifaa vya kupikia), Chimpumu, dengerua, gongo (aina ya pombe), kuuza sura, kindumbwendumbwe, mchakamchaka, sadakarawe, Pole, Chanda, Askari, Hakuna matata, Jambo, K(V)ipusa, swahiba, Shoga, Basha, waubani na mengine meeeengi.