Je kiungulia ni ishara ya saratani?

RUCCI

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2011
Posts
1,701
Reaction score
1,714


Madaktari mjini Devon wanaunga mkono kampeni mpya inayowaagiza raia kuwatembelea madaktari wao iwapo wanahisi kuwa na kiungulia kwa siku kadhaa kwa kuwa huenda ikawa ishara ya ugonjwa wa saratani.

Zaidi ya watu 10,000 hufariki kutokana na saratani ya tumbo ama ile ya koromeo kila mwaka nchini Uingereza ambayo ni sawa na watu 28 kila siku.

kampeni hiyo inayofanywa na idara ya afya ya uma nchini Uingereza inasema watu sita kati ya kumi hawajui kwamba kiungulia huenda kikawa ishara ya Saratani.

Pia inasema kuwa karibia nusu ya watu hutembelea madaktari wao iwapo wanaugua kiungulia kwa wiki tatu ama zaidi.

Daktari Tom Debenham kutoka Devon na mkuu wa kliniki za kazkazini,mashariki na magharibi mwa Devon anasema kuwa watu wanafaa kuelezwa kuhusu uhusiano kati ya kiungulia na saratani.

''Iwapo unahisi kiungulia kila mara,nenda ukamuone daktari ,hata iwapo unatumia dawa na unahisi zinakusaidia''.

''Huenda si kitu chochote hatari lakini iwapo ni saratani kuigundua mapema inakuwa rahisi kuitibu.'',alisema daktari huyo.

Watu pia wameagizwa kuwatembelea madaktari wao iwapo kila wanapomeza chakula wanahisi kwamba chakula kinazuiliwa katika koromeo.

Source:BBC
 
Duh! Hizi tafiti kila siku ni mpya,ila kiungulia ni dalili ya vidonda vya tumbo,sasa labda mtu anakuwa na vidonda vya tumbo muda mrefu hatimaye vinageuka vinakuwa ni saratani.
 
Duh! Hizi tafiti kila siku ni mpya,ila kiungulia ni dalili ya vidonda vya tumbo,sasa labda mtu anakuwa na vidonda vya tumbo muda mrefu hatimaye vinageuka vinakuwa ni saratani.

Umeelewa vizuri that's the point
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…