JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
Baada ya Serikali Kutangaza kuwa Wasafiri wote wanaokwenda nje ya Nchi wanapimwa maambukizi ya #CoronaVirus kwa gharama ya Dola za Kimarekani 100 ambazo ni sawa na Tsh. 231,900
Kupitia mitando ya Kijamii Watanzania wamehoji uhalisia wa tozo hiyo na kuelezea kuwa haina uhalisia
Mfano Mfanyabiashara anayekwenda Nairobi Kenya kwa basi nauli yake ni ndogo kuliko gharama za kupima ugonjwa huo
Aidha, wapo waliosema kuwa gharama hizi zitawakatisha tamaa Watalii kurudi tena nchini kwani wapo ambao kwenye Nchi zao kipimo ni Euro 60 tu ambayo ni sawa na Tsh. 170,000
Upvote
0