Je, kiwanja cha Futi 50 Kwa 40 kinajenga vyumba vingapi? Wataalamu tujuzane

Je, kiwanja cha Futi 50 Kwa 40 kinajenga vyumba vingapi? Wataalamu tujuzane

Meneja CoLtd

Senior Member
Joined
Mar 6, 2021
Posts
122
Reaction score
143
Habari zenu wana JF!

Baada ya kuwaza sana kuhusu hivi viwanja vya mikopo vinavyouzwa, vyenye ukubwa wa Futi 50 Kwa 40 kama je, vinatosha kujenga nyumba?

Kwangu Mimi nimeona itatosha endapo pale mnunuzi atakua hana mambo mengi.

Kama vile kujenga vyumba vinne, choo cha ndani na sebule Kwa vipimo hivi nilivyotumia.

Mafundi naomba mnipe msaada hapa kwenye hii ramani yangu, je inakidhi vigezo?

IMG-20241201-WA0001_1.jpg
 
Unajengea nyumba nzuri, unakosa nafasi hata ya kutosha.

Ukipiga ukuta unajikuta upo gerezani nafasi huna na hewa hakuna.

Serikari ingepiga marufuku viwanja vya namna hii
 
Habari zenu wana JF!
Baada ya kuwaza sana kuhusu hivi viwanja vya mikopo vinavyouzwa, vyenye ukubwa wa Futi 50 Kwa 40 kama je, vinatosha kujenga nyumba?

Kwangu Mimi nimeona itatosha endapo pale mnunuzi atakua hana mambo mengi.

Kama vile kujenga vyumba vinne, choo cha ndani na sebule Kwa vipimo hivi nilivyotumia.
mafundi naomba mnipe msaada hapa kwenye hii ramani yangu, je inakidhi vigezo?View attachment 3166686
Kiwanja cha futi 40 kwa futi 50 ni sawa na kiwanja cha mita 12 kwa mita 15.

Kwenye mita 12 ukitoa nafasi ya njia ya mita moja moja kushoto na kulia inabaki mita 10 japo kuwa kama unataka uombee kibali cha ujenzi, nafasi ya njia kushoto na kulia inabidi isipungue mita 1.5

Nyumba ya vyumba vitatu inakaa ila vyumba vyake vitakuwa ni vya wastani, na pia vitu kama store sijui pray room inabidi visiwepo maana katika hilo hilo eneo inabidi iachwe nafasi ya karo/makaro ya vyoo
 
Hizo ni 180 sq.metres:Kwa Nyumba ya Makazi inatosha,unahitaji architect Makini ambapo Sq.m 100 inakupa Vitu Mhimu:Living room,Jiko na store,Vyumba vya Kulala 2 Vyote Masta, Canopy Safi.Nafasi ya Maegesho pia Gari 1.Usicomplicate Maisha.Nina Kiwanja 1 Mkoani sq.metre 1000 nimejenga Nyumba sq.m 100 nafasi kubwa imebaki ndani ya Fensi kila siku nina headache Eneo nitalifanyia nini.Mfanyakazi analima bustani.
 
Back
Top Bottom