Salamu kwenu wataalamu wote! Hata wadau wote wa jukwaa hili.
Naomba kujua, je kondomu za kiume kutoka kampuni gani angalau ni sahihi kwa (a) kuzuia virusi vya UKIMWI na (b) kuzuia mimba.
Naomba ushauri kwa kuwa kumekuwa na tishio la kondomu bandia, kampuni kadhaa matangazo lukuki, huku kila kampuni ikija na mbwembwe zake kama harufu za kuvutia n.k.
Kwa bahati mbaya, watumiaji wamekuwa wakitoa malamiko ikiwamo kuwashwa, kuvimba kwa sehemu za siri baada ya matumizi. Naomba majibu toka kwako.
Condoms ni contraceptives..condoms hazizuii ukimwi,zinazozuia magonjwa mengine ya gono,ila labda kwa itumike kiusahihi.