Infiltrator
JF-Expert Member
- May 13, 2017
- 211
- 339
sijaelewa, kwa nini uko against wanawake (watoto) kusaidiwa ''pedi'' ? ...
Upo sahihi kabisa
Sidhani kama umeelewa hoja yangu vizuri. Sipo dhidi ya watoto wa kike kusaidiwa pedi, hilo ni jambo jema na la kibinadamu. Hakuna mwenye akili timamu anayeweza kupinga msaada kwa wanafunzi wa kike, hasa wenye mahitaji maalum.
Hoja yangu ni kuhusu vipaumbele na hadhi ya nafasi ya ubunge. Mbunge ni mtunga sera, msimamizi wa bajeti na mwakilishi wa wananchi katika masuala makubwa ya maendeleo. Tunatarajia aoneshe mchango wake katika kutatua changamoto za kimfumo, si kujinasibu kwa matukio madogo yanayoweza kufanywa na viongozi wa ngazi za chini au taasisi za kijamii.
Aisha, tatizo zaidi linakuja pale tukio linapogeuzwa ajenda ya kujitafutia sifa kana kwamba huo ndio uzito wa kazi ya ubunge.
Kwa kifupi, sipingi msaada. Nahoji uongozi na mwelekeo wa vipaumbele.
Mimi nagawa sanda kwenye Jimbo langu la masasi.sijaelewa, kwa nini uko against wanawake (watoto) kusaidiwa ''pedi'' ? kwa nini ni jambo baya hadi ufure namna hiyo? ...
Hao walevi wa Dar hawaelewi mengi tu ya maana yanayofanyika hapa duniani.sijaelewa, kwa nini uko against wanawake (watoto) kusaidiwa ''pedi'' ? kwa nini ni jambo baya hadi ufure namna hiyo? ...
Charity begins at home.Nimestaajabu kuona mtu mwenye hadhi ya ubunge akijihusisha na matukio yanayofaa kufanywa na mjumbe wa nyumba kumi, huku akijinasibu mitandaoni.
Je, hili ni “funika kombe mwanaharamu apite” au ni dharau kwa wananchi? Je, wabunge mnadhani hatujitambui?
Mbali na nafasi yake ya ubunge, huyo mshangazi ni Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Dodoma.
Wanawake wa Dodoma, kama huyu ndiye kiongozi wenu, kuna haja kubwa ya kujitafakari; kwa kifupi, hajitambui kabisa!
Hali kama hii inaleta maswali makubwa kuhusu uwazi na vipaumbele vya ziara za wabunge.
Wananchi wanatarajia uwajibikaji, si matukio yanayoonyesha ukosefu wa utambuzi hadharani.
Neema Majule (Mshangazi), jitafakari sana; matukio yako ya mchongo hayana nafasi katika hadhi ya ubunge.