Travis Walker
JF-Expert Member
- Apr 10, 2017
- 323
- 334
Habari vijana.
Leo nakuja na mada nyengine inayovutia ambayo tutazungumza kuhusu JINAMIZI .
Watu wengi wanaamini ya kwamba jinamizi ni jini ama mzimu usionekana unaosumbua watu wakati wapo katika usingizi.Ila ukweli hakuna kitu kiitwacho jinamizi.Hali ambayo watu wanafikiria kuwa ni jinamizi inaitwa SLEEP PARALYSE.
JEE NI NINI SLEEP PARALAYSE?
Sleep paralyse ni hali inayotokea wakati unapooanza kulala yaani kilepe au unaposhituka kutoka katika usingizi.Hali humfanya mtu kujihisi mwili wake haufanyi kazi na pia kushindwa kuongea wakati ameshituka yupo macho.Anaona kila kitu ila anashindwa kutukusa hata kidole kwa muda wa sekunde ama dakika chache.
KWANINI SLEEP PARALYSE HUTOKEA?
Wakati umelala, mwili hubadilishana baina ya mizunguko miwili ya usingizi ambayo inatwa REM (Rapid Eyes Movement) na NREM (Non Rapid Eyes Movement).
Mzunguko mmoja wa REM na NREM huchukua dakika 90 mpaka kuisha kwake.Mzunguko wa NREM huanza fasi wakati ukilala na huchukua asilimia 75% za usingizi wote.Wakati wa mzunguko wa NREM mwili wako hupumzika na kujijenga tena.Unapomalizika mzunguko huu wa NREM huingia mzunguko unaoitwa REM.Katika mzunguko huu macho yako huzunguka kwa kasi wakati yamefumba na hapo ndipo ulimwengu wa ndoto huanza.Pia mwili wote huzimika katika mzunguko REM na kushindwa kufanya kazi.Sasa ikitokezea unashituka kabla ya mzunguko wa REM haujamaliza unajikuta mwili wako wote na kila kiungo kinashindwa kufanya kazi na ndipo huanza kuchanganyikiwa na kuhisi ni jini ama pepo.Na mara nyingi watu hushituka kabla ya dakika chache mzunguko huu kuishia na Ndio maana kitendo chenyewe hutokea kwa kuda mchache.
Kama ingelikuwa mtu anashituka nusu saa kabla ya mzunguko kuishia basi mtu angelikufa na engelikuwa ni tatizo kubwa duniani.
TIBA YA UGONJWA HUU NI IPI?
Kwa kweli huu si ugonjwa na ni hali ya kawaida , na kama si ugonjwa hatuhitaji tiba ila kuna mambo yafuatayo husababisha hali hii kutokea hivyo tunashauri kuepukana nayo.
1.Usijitishe wakati wa kulala kwa maana ubongo hubakia na hofu na hivyo hushituka pasi
na kufuata order.
2.Pia unatakiwa kutafuta njia ya kupunguza street na mfadhaiko katika maisha yako.
3.Pia unatakiwa ulale katika mazingira yenye amani ili kuondosha hofu na stress katika mwili.
4.Usilale sehemu yenye joto sana kwasababu inasabisha ubongo kuwepo makini kila wakati na hivyo hushituka mara kwa mara.
5.Pia unatakiwa ulale angalau masaa sita kila usiku.