The Sheriff
JF-Expert Member
- Oct 10, 2019
- 747
- 2,112
Kuna jambo nimelikumbuka wakati nafanya mazungumzo na wafanyakazi wenzangu leo. Tulikuwa tukijikumbusha visanga na mambo mbalimbali ya miaka ya nyuma wakati tukisoma.
Ni kuhusu kujaladia madaftari. Hii kwa walimu wengi ilikuwa ni sharti muhimu; yaani akiingia darasani anaweza kuamua tu kukagua madaftari kama yamejaladiwa na yeyote anayepatikana na hatia anaambulia mikwaju kadhaa ya kumkumbusha kuwa “msafi”.
Wakati mwingine ilikuwa kwamba tukikusanya madaftari kwa ajili ya mwalimu kufanya usahihishaji, yalikuwa yanaweza kurudi yakiwa katika makundi mawili – yaliyojaladiwa na yasiyojaladiwa. Hapo sasa wenye madaftari yaliyo “uchi” wanaadhibiwa ili “kuwakumbusha” umuhimu wa kuwa “wasafi”.
Haikujalisha daftari lako lilikuwa safi kiasi gani, jalada ilikuwa ndiyo kipimo cha usafi kwa mujibu wa walimu wa enzi hizo. Sina hakika sana kama bado huu utaratibu bado unaishi.
Mimi nilikuwa natumia zaidi kalenda zilizopitwa na wakati. Upande mweupe usio na picha ndiyo nilikuwa napendelea zaidi utazamane na walimu ili kuthibibitisha “usafi” wangu. Wakati mwingine nilitumia magazeti.
Mpaka sasa sijajua kwanini kulikuwa na ulazima wa kujaladia; tena vikiambatana na kulazimishwa kwa bakora.
Hebu na wewe tupatie experience yako kuhusu hili. Karibu.