Je, kujengea nondo kwenye frem ya duka kunahitaji kibali manispaa?

herman3

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2015
Posts
556
Reaction score
736
Habari ndugu.

Nina fremu ya biashara nauza maji na vinywaji kwa bei ya jumla lakini kwa sababu ya ufinyu wa nafasi nimeamua kujengea nondo mbele ya frem ili angalau kuweka bidhaa ambazo zimekosa nafasi ndani (nadhani wengi tumeona maduka mengi ya vinywaji wanavyofanya.).

Sasa, kama kichwa cha mada kilivyo naomba kufahamu je hili jambo la kutakiwa kuwa na kibali cha manispaa lipo kisheria? Maana ninasumbuana na watu wa serikali za mtaa wanataka nisimamishe ujenzi hadi nipate kibali cha manispaa ili kujengea nondo kwenye fremu yangu ya biashara Kinondoni.
 
Ndio mkuu, hiyo ipo kisheria kabisa. Na kupata kibali malipo ni Kati ya 20,000/- au 50,000/- sikumbuki vizuri.
 
Ahsante sana, naomba kufahamu hatua zipoje? Naanzia ofisi gani manispaa?
 
Anza na hao hao Serkali ya Mtaa, hao ndo wanakutambua, means watakuandikia barua then utaenda Manispaa.
 
Ahsante sana, naomba kufahamu hatua zipoje? Naanzia ofisi gani manispaa?
Sina uzoefu mkuu, mie huwa Nina watu wangu(wahandisi) ndio huwa wananisaidia kuharakisha upatikanaji wake.
Kwa ushauri tu, ukienda manispaa/halmashauri dawati la maulizo naamini utaelekezwa.
 
Ahsante mkuu
 
Inaitajii kibalii mkuu ,kariako nimeshuhudia ktk frem mpya zilizotengenezwa ,mwenye frem kabla yakuanza ujenzi alichukua kibali cha ujenzi utakaokamilika kwa upande wake kwa miez minne baada ya hapo atakaendelelea na chcht atakaepanga ktk frem bac atawajibika kutafuta kibali ili aendelee na anachokitakaa ,,ht km unawekaa Dari juu ya frem wakikukamta na una kibali bac watadilii nawee.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duuh, sawa mkuu nimekuelewa sikuwa nafahamu kuhusu hilo, nilidhani wanataka kunionea ili niwape chochote hivyo, ikabidi nitafute kwanza taarifa sahihi ili nipate uhakika.
 
Back
Top Bottom